Waandamanaji wanaompinga rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wameagiza kusitishwa kwa maandamano hayo kwa siku mbili.
Msemaji wa vyama vya kiraia amesema kuwa hatua hiyo itazipa fursa familia za wale waliouawa katika maandamano hayo kuomboleza.
Takriban watu sita wamefariki tangu maandamano hayo yaanze jumapili iliopita.
Siku ya Ijumaa usiku,maafisa wawili wa polisi na mtu mmoja waliuawa katika shambulizi la guruneti.
Awali rais wa taifa hilo aliwaonya maafisa wa vyama vya kiraia kwamba ataawadhibu.
Wapinzani wamemshtumu kwa kukiuka katiba.
No comments:
Post a Comment