Usain Bolt hana tatizo la kushindana dhidi ya Justin Gatlin kwa kuwa anahisi kwamba marufuku ya miaka minne aliyopewa ilikuwa ya haki.
Bingwa huyo mara mbili wa michezo ya Olimpiki hivi majuzi alilalama kuhusu mwanariadha mwengine wa mbio fupi kutoka Marekani Tyson Gay ambaye alipigwa marufuku kwa mwaka mmoja baada ya kupatikana amekula dawa za kusisimua misuli.
''Marufuku aliyopewa Tyson ilikuwa haitoshi na kutuma ujumbe mbaya'', alisema Bolt. ''Justin Gutlin alipigwa marufuku na akaihudumia kwa hivyo sina shida naye'',.
Mkimbiaji huyo wa mbio fupi kutoka Jamaica atapambana na wawili hao wikendi hii katika mbio za 4 mara 100 katika mashindano ya relay huko Bahamas.
No comments:
Post a Comment