Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maafikiano hayo.
 |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu muafaka uliofikiwa kufuatia mgomo wa madereva uliofanyika ofisi ya waziri mkuu kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.
|
 |
Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema Serikali
imetimiza masharti ya madereva kwa kuunda kamati ya kushughulikia kero
na matatizo ya madereva ambayo inatarajia kuanza kazi yake Ijumaa.
Hatua
hiyo imekuja baada ya madereva hao kufanya mgomo kwa muda ukiwa na
lengo la kushinikiza kutatuliwa kwa madai yao mbalimbali yakiwemo ya
kimikataba baina yao na wamiliki wao.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Makonda alisema kamati hiyo itakuwa ya kudumu
ambayo itakuwa ikishughulikia kero na matatizo ya barabarani nchini.
Alisema kamati
hiyo ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Uchukuzi, Dk.Shabaan
Mwinjaka itakuwa na wajumbe mbalimbali kutoka akiwemo Katibu Mkuu
Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
wawakilishi watatu kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi ya Tanzania
(Taboa) na Kakoa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani na washiriki watano kutoka chama cha madereva nchini.
Makonda alisema lengo la kuteua wajumbe kutoka Serikalini na taasisi hizo ni kutokana na uwepo wa uhusiano mkubwa kati yao na madereva hao.
"Watu
hawa wataweza kushirikiana vema na kutatua kero hizi kutokana na wao
katika shughuli zao zinahusiana moja kwa moja hivyo kuweza kuendesha
kamati hii vizuri.
"Tunataka watu kushughulikia jambo kabla
halijakuwa tatizo hivyo kamati hii itakuwa ikikutana mara kwa mara
katika kushughulikia maswala mbalimbali kuhusiana na madereva na
barabara kwa ujumla ili kuondoa kero mbalimbali ," alisema Makonda.
Baadhi
ya agenda zitakazo fanyiwakazi mara baada ya kamati hiyo kuanza kazi ni
pamoja na madai ya madereva hao likiwemo la mikataba ambayo inadaiwa
kuwa yanamuda wa miaka kumi, kutokuwa na utaratibu wa kuwalipa madereva
hata wakipatwa na matatizo.
Alitaja agenda nyingine ni za faini sizizo
za mpangilio wanazotozwa madereva hao wakiwa kwenye shughuli zao, suala
la kurudi shuleni kila wanapohitaji kurinyu leseni zao na kukaa kwenye
mizani kwa muda mrefu pamoja na taratibu nyingine ambazo zinakuwa kero
katika shughuli zao.
Makonda alisema wakati walipowasili Ofisi
ya Waziri Mkuu, walikuta wawakilishi kutoka Wizara ya Uchukuzi, Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Taboa, Kakoa,
Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Wizara ya Kazi na Ajira, ambapo
walikaa na kukubaliana kuunda kamati hiyo.
Alisema pamoja na
uwamuzi huo wa kuunda kamati hiyo Serikali haitachagua wala kuteua
wawakilishi kutoka upande wa madereva ili kuwapa fursa madereva hao
kuweza kuwachagua watu ambao wanaaamini zaidi.
Kutokana na
uwamuzi huo wa kuundwa kwa kamati hiyo ya kudumu Makonda alisema
hakutakuwa na mgomo tena kwani kamati hiyo itaweza kidhi mahitaji ya
kila upande kwa makubaliano ya wajumbe wake.
"Leo, asubuhi
kama nilivyo waahidi madereva tulikwenda na wawakilishi waio wakiwemo
viongozi wao hadi kwa Waziri Mkuu ili kuangalia kama yale tuliyo
yahitaji jana yametekelezwa na hapo tuliweza kupata muafaka na kuunda
kamati hiyo.
"Hivyo
kuanzia sasa hakutakuwa na mgomo na hatutakuwa na mgomo tena kwani
madai yaetu tunaimani yatafanyiwa kazi ipasavyo.Na ndio maana tukatoa
nafasi kwa madereva kuwa na wajumbe wengi zai ili kuwa na nguvu zaidi
kuliko wajumbe wengine katika kutatua kero zao," alisema makonda.
Makonda
alisema kuwa lengo la kuundwa kwa kamati hiyo si kumaliza tatizo hilo
bali ni kuzima moto wa milele kwenye kero za madereva wote nchini.
Akizungumzia
kuhusu baadhi ya viongozi wakiwemo wanasiasa wanaotumia migogoro kama
fursa ya kutafuta umaarufu Makonda alisema si jambo jema na kuwataka
viongozi hao hususani vijana kujifikiria kutoa msaada katika jamii na si
kutafuta umaarufu.
"Niwaombe
tu vijana wenzangu najua wazee hawatobadilika na badala yake
watuangalie vijana tunavyofanya kazi hivyo tuhakikishe kutokuwa kikwazo
kwa mwenzake kwa kugeuza kila anachofanya mwenzake ni jambo baya,"
alisema Makonda. (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
|
No comments:
Post a Comment