TANGAZO


Tuesday, April 28, 2015

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mlimani wapatiwa mafunzo

*Ni katika kuadhimisha siku ya Afya na usalama
Mkuu wa  Kitengo cha Usalama  Barabarani wa Mkoa wa kipolisi  Kinondoni, Kamanda Solomoni Mwangamilo (wapili toka kushoto) na Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare (kushoto) pamoja na Mkaguzi wa Usalama na Afya Sehemu za Kazi wa OSHA, Emannuel Lyozia (kulia) wakitoa heshima ya kuwakumbuka Wananchi waliokufa kutokana na ajali za barabarani wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani.
Mkuu wa  Kitengo cha Usalama  Barabarani wa Mkoa wa kipolisi  Kinondoni, Kamanda Solomoni Mwangamilo, akiwaelimisha kuhusiana na umuhimu wa kuwa makini watumiapo vyombo vya moto barabarani wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani.


Mkuu wa  Kitengo cha Usalama  Barabarani wa Mkoa wa kipolisi  Kinondoni, Kamanda Solomoni Mwangamilo (wa tatu toka kushoto) na Inspekta Msaidizi wa Usalama Barabarani Elizabeth Ndambara (kulia) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) wakimsikiliza jambo Ofisa Mkuu wa  Idara Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimani, Mariam Mrisho (kushoto) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango kwa ajili ya kutoa elimu kwa madereva wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwanaidi Khamis mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam (kushoto) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango kwa ajili ya kutoa elimu kwa madereva wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Ofisa polisi wa Usalama Barabarani (CPL) Wilbart Binamungwe (kushoto) akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mlimani jijini Dar es Salaam jinsi ya kuvuka barabara, wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam, wakisoma mabango yaliyoshikiliwa na wanafunzi wenzie yenye ujumbe wa kusisitiza madereva kutokuvunja sheria za barabarani. Wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Polisi wa Usalama Barabarani (CPL) Wilbart Binamungwe akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mlimani jijini Dar es Salaam jinsi ya kufuata sheria za kuvuka barabara, wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi  wa Shule ya Msingi ya Mlimani jijini Dar es Salaam, Simon Miraji akimuuliza swali  juu ya sheria za  uvukaji barabara Ofisa polisi wa Usalama Barabarani (CPL) Wilbart Binamungwe. Wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania, Happiness Paul.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mlimani jijini Dar es Salaam wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kusisitiza madereva wanaotumia vyombo vya moto kufuata sheria za barabarani watumiapo vyombo hivyo wakati wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Kazini Duniani. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ilifanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam leo wameadhimisha siku ya Afya na Usalama mahala pa kazi duniani kwa kupatiwa mafunzo ya usalama sehemu za kazi na usalama barabarani  na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Kanda ya Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo elimu hii pia itatolewa katika shule za msingi zingine jijini mapema wiki hii.

Mafunzo hayo yaliyotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo yalionekana kuwavutia wanafunzi wa shule hiyo ambao  pia walishiriki katika mazoezi ya kukabiliana na  majanga mbalimbali yanayojitokeza kwa dharura.

Akiongea juu ya mafunzo Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare,amesema Vodacom ikiwa ni kampuni inayozingatia usalama wa wafanyakazi wake na watanzania wote kwa ujumla imeamua kutoa mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi ikiamini kuwa wao ndio wafanyakazi wa baadaye ambao ndio tegemeo la kukua kwa uchumi wetu.
Alisema mafunzo haya yanalenga kuwafahamisha masuala ya usalama mahala pa kazi,ikizingatiwa kuwa wao pia wanaishi katika jamii kama watu wengine wote na wana  haki ya kufahamu usalama pia wengi wao ni watumiaji wa barabara wakati wa kwenda na kurudi shuleni hivyo  wanapaswa kuelewa sheria za usalama barabarani kwa manufaa yao.

“Tumeona pia kuna umuhimu kwa wanafunzi hawa kujua alama mbali mbali za barabarani pamoja na matumizi yake mbali na kuishia kuziona tu kwa macho. Kama suala la usalama barabarani lazima lipewe kipaumbele kwani kama tujuavyo jiji la Dar es Salaam lina changamoto nyingi ukizingatia magari sasa yamekuwa mengi kitu na matumizi ya barabara yanachanganya watu wengi na kusababisha kuwepo na ajali nyingi za barabarani”.Alisema.

Aliongeza kuwa Vodacom kwa kushirikiana na Baraza la Usalama barabarani na jeshi la Polisi imekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeni za usalama barabarani  ya ‘Wait to Send’ na leo imefurahi kampeni hii badala ya kuwafikia madereva pekee sasa imewafikia na wanafunzi ambao ni watumiaji wakubwa wa barabara.
Kwa upande wake Mkuu wa  Kitengo cha Usalama  barabarani wa Mkoa wa kipolisi  Kinondoni,, Kamanda Solomoni Mwangamilo amesema kuwa suala la usalama barabarani linawahusu watanzania ili kupunguza matukio ya ajali na aliipongeza Vodacom kwa kuwa mstari wa mbele kulivalia njuga tatizo hili.

“Nawapongeza kwa jitihada zenu katika kuunga mkono juhudi za serikali kukabiliana na wimbi la ajali nchini na mmefanya jambo la maana kupeleka elimu ya usalama barabarani mashuleni kwa kuwa wanafunzi hawa wengi wao wanatumia barabara wakati wa kuja shuleni hivyo hawapaswi kubaki nyuma”.Alisema.

No comments:

Post a Comment