Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard
Kayombo akitoa neno kuwakaribisha wageni katika mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa
Vyuo vya Kodi Afrika uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 50 kutoka katika taasisi
za kodi barani Afrika, Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi za Kodi Afrika (ATAF), leo Jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Kodi Tanzani (ITA) Prof. Isaiah Jairo akiongea na
wajumbe wa mkutano huo na kueleza namna utakavyosaidia katika kuzijengea uwezo
Taasisi za ukusanyaji kodi Afrika hivyo kuweza kuinua uchumi wa Mataifa mengi
ya Afrika.
Mkurugenzi
wa Ujengaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi
akiwaeleza wajumbe wa Mkutano huo namna Kamati hiyo inavyoshirikiana na Taasisi
za Kodi Afrika katika kuzijengea Taasisi hizo uwezo wa Kiutendaji na kusaidia
nchi wanachama kushiriki kuwa na sera ya pamoja ya masuala ya Kodi ili kuongeza
ufanisi katika ukusanyaji kodi.
Naibu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba Akiongea na wajumbe waliohudhuria Mkutano huo
namna Tanzania ilivyofurahishwa na kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Kwanza wa
wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Afrika
na kuwataka wajumbe kutumia fursa hiyo kujifunza masuala mbalimbali katika
sekta hiyo ya ukusanyaji kodi kwani ni moja ya mhimili muhimu wa maendeleo kwa
Mataifa mengi duniani.
Wakuu
wa Vyuo vya Uongozi wa Kodi Barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi
Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi
akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo wa kwanza unaofanyika Nchini Tanzania.
Mkurugenzi
Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi
akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo wa kwanza unaofanyika Nchini Tanzania. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)
No comments:
Post a Comment