TANGAZO


Thursday, April 30, 2015

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal arejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa Sadc jijini Harare, Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishara ya makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini Harare, Zimbabwe. Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati waliosimama), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC jana. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini Harare, Zimbabwe jana April, 29, 2015. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwapungia wenyeji wake wakati akianza safari ya kurejea nyumbani. (Picha zote na OMR)

No comments:

Post a Comment