TANGAZO


Thursday, April 30, 2015

CLOUDS FM yashinda tena Tuzo ya Ubora ya Super Brand kwa mara ya Tatu Afrika Mashariki

Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za viwango, kutoka shoto ni Bi. Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta ya PetrolFuel, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce Mhaville, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya Alliance Insurance.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki, Bwana Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na Mkuu wa kitengo cha huduma, Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi Fauzia Kullane.
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki, Bwana Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo bora za viwango hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki, Bwana Jawad Jaffer.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group, Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV, Bwa. Godwin Gondwe

Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.

Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki, Jawad Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.

Utafiti huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini  Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.

Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000 zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.

No comments:

Post a Comment