TANGAZO


Sunday, April 12, 2015

Maalim Seif Sharif, aweka mawe ya msingi na kupandisha bendera katika matawi na Baraza sita za CUF Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika baraza ya CUF ya WENYE WIVU WAJINYONGE katika eneo la Kitope, Mkaratini leo. 
Vijana wa baraza ya HATUDANGANYIKI  ya Kiwengwa Cairo wakimsikiliza Maalim Seif wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika baraza hiyo leo. (Picha zote na OMKR)

Na Hassan Hamad (OMKR)
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameweka mawe ya msingi na kupandisha bendera katika matawi na barza sita za CUF ndani ya Jimbo Kitope Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja. 

Matawi na barza alizoweka mawe ya msingi ni pamoja na Kiombamvua, Mkaratini, Mgambo, Kilombero, Kipandoni na Kiwengwa Cairo.

Hata hivyo, mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike katika viwanja vya Kipandoni umehairishwa, kwa madai kuwa haukupata kibali kutoka kwa jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment