TANGAZO


Friday, February 6, 2015

Umoja wa Wazazi wa CCM Wilaya ya Ilala wafanya Kongamano la Wajibu wao kwa Katiba iliyopendekezwa Dar es Salaam leo


 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar,  Najma Giga, akisalimiana na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale baada ya kuwasili kwenye kongamano hilo.
Ukaribisho ukiendelea
Viongozi mbalimbali kutoka Makao Makuu ya Jumuiya hiyo wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar,  Najma Giga,  akionesha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa mada katika Kongamano la jumuiya hiyo lililoandaliwa na jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala lililohusu wajibu wa jumuiya ya wazazi kwa katiba iliyopendekezwa. Kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala, Lugano Mwafongo
 Katibu wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala, Lugano Mwafongo (kulia), akizungumza katika kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale na  Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar,  Najma Giga,
 Katibu wa Jumuiya hiyo, Mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje Mohamed Cholaje (kulia), akizungumza katika Kongamano hilo.
 Viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Wanachama wa jumuiya hiyo kutoka Mkoa wa Kusini Unguja wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye kongamano hilo.
 Wanajumuiya hiyo kutoka Wilaya ya Ilala wakijumuika katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanachama wa jumuiya hiyo kutoka Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa kwenye kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale
WANAJUMUIA ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuwaelimisha wananchi wengine umuhimu wa kuipigia kura ya ndio katiba iliyopendekezwa ifikapo Aprili 30 mwaka huu.
Mwito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Zanzibar Najma Giga,  Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa mada katika Kongamano la jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala lililohusu wajibu wa jumuiya ya wazazi kwa katiba iliyopendekezwa.
Giga alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo lililowajumuisha wanachama wa jumuiya hiyo 60 kutoka mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar ambalo liliandaliwa na jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala.

"Kila mwanachama wa jumuiya ana wajibu wa kutekeleza maagizo yanayotolewa mara kwa mara na CCM kwa jumuiya hiyo ili kutekeleza ilani ya chama chetu" alisema Giga.

Alisema jumuiya hiyo imeundwa kwa mujibu wa katiba ya Chama Cha Mapinduzi sehemu ya nne ibara ya 129 (1) (C), (3), (4) na (5) ambapo umoja huo ni miongoni mwa jumuiya tatu za CCM.

Alisema jumuiya hiyo hivi sasa inapaswa kujipanga vizuri kutokana na kuwepo mambo makubwa mawili ya kuipigia kura ya ndio katiba hiyo na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Katibu wa jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala, Lugano Mwafongo alisema jumuiya hiyo katika wilaya yake wamejipanga kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola kwa kuwa ni chama pekee kinachokubalika na wananchi.

"Katika wilaya ya Ilala tumejipanga vizuri na kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola na ndio maana tumekuwa na uhusiano wa kubadirishana mawazo na wenzetu kutoka nje ya wilaya yetu kama tulivyokutana na wanajumuia hawa kutoka Mkoa wa Kusini Unguja kuja kubadilishana nao uzoefu wa mambo mbalimbali na mchakato wa upigaji kura ya maoni ya katika iliyopendekezwa" alisema Mwafongo.
Alisema ushirikiano huo umekuwa na nguvu kutoka umoja walionao baina ya wanajumuiya na viongozi wao kuanzia ngazi ya matawi, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.

Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje Mohamed Cholaje alisema tangu wachaguliwe kuwa viongozi wa jumuiya hiyo imepata mafanikio makubwa na kuwa wameweza kuwa na orodha ya wanajumuiya kuanzia ngazi ya shina baada ya kuweka daftari maalumu la kuwasajili wanachama. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment