TANGAZO


Wednesday, February 11, 2015

Rais wa Caf ataka kuendeleza muda wake

Mkutano wa shirikisho la soka barani Afrika Caf
Rais wa shirikisho la soka barani Africa CAF Issa Hayatou anataka kubadilisha sheria za shirikisho hilo kuhusu umri ili aendelea kuhudumu hadi muongo mwengine.
Sheria za Caf zinasema kuwa maafisa ambao wamefika umri wa miaka 70 wanafaa kustaafu lakini mabadiliko hayo yanatarajiwa kupendekezwa na kujadiliwa katika mkutano wa mwezi Aprili.
Hayatou mwenye umri wa miaka 68 anahudumu katika muhula wake wa saba afisini baada ya kuchaguliwa mwaka wa 1998.
Kombe la Caf
''Fifa haina kiwango cha umri unaohitajika kwa wana kamati wake kwa hivyo Caf inapendekeza mabadiliko hayo ili yawe sambamba na wanakamati hao'',alisema mwanachama wa kamati hiyo Kwesi Nyantakyi.
Hayatou anatarajiwa kuhudumu hadi mwaka 2017 na anawania kupewa miaka meingine minne hadi mwaka 2021 ambapo atakuwa na umri wa miaka 75.
Sheria ya Caf inasema kwamba wakati wa kuchaguliwa kwao ,wagombea wote walioteuliwa katika kamati ya Caf ni lazima wawe wanachama wa mashiririkisho yao na wawe chini ya miaka 70.

No comments:

Post a Comment