Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Caf, Issa Hayatou anataka kubadili sheria za chombo hicho kuhusu umri wa mwisho katika uongozi, ili aweze kuendelea kugombea.
Caf inataka maafisa wanapotimiza miaka 70 kujiuzulu madaraka lakini mabadiliko yatapendekezwa na kujadiliwa katika mkutano wa shirikisho hilo mwezi Aprili.
Hayatou, mwenye umri wa miaka 68, yuko katika muhula wa saba katika utawala wa Caf, akiwa amechaguliwa mwaka 1998.
"Fifa haina kikomo cha umri kwa wajumbe wake wa kamati kwa hiyo Caf inataka kuleta hoja hiyo kwa maafisa wake," amesema mjumbe wa kamati kuu ya Caf Kwesi Nyantakyi.
Utawala wa sasa wa Hayatou unaishia mwaka 2017 na anataka miaka minne zaidi hadi mwaka 2021, atakapotimiza umri wa miaka 75.
Kifungu katika katiba ya Caf inasema "katika wakati wao wa uchaguzi, wagombea wote waliopendekezwa kuingia katika kamati kuu ya Caf lazima wawe wajumbe wa vyama vya soka katika nchi zao na lazima wewe chini ya umri wa miaka 70."
Lakini kifungu hiki kinaweza kuondolewa endapo pendekezo la kufuta ukomo wa umri litapitishwa katika mkutano mkuu wa Caf, kama linavyotarajiwa.
Mabadiliko ya sheria hii inafuatia mafanikio katika miaka ya hivi karibuni katika kupitisha vifungu vya katiba vinavyopunguza upinzani katika utawala wa Hayatou.
Awali Caf iliweka sheria kwamba wagombea wa nafasi ya urais wanaweza kutoka ndani ya kamati yake ya utendaji, kipengele ambacho kilidhibitiwa kwa karibu na Hayatou. Fifa haina sharti hilo.
Hayatou mzaliwa wa Cameroon, afisa wa zamani wa riadha, tayari ni mjumbe mwandamizi wa muda mrefu katika muundo wa Fifa, ambako anahudumu kama makamu wa rais, na anakabiliwa na wapinzani wachache kutoka Afrika katika nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment