Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akiongoza kikao cha siku moja cha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa wizara ya hiyo, kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu, Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Idara zake mbali mbali wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Abdilah Jihadi Hassan (hayupo pichani) alipokuwa akitoa taarifa ya Wizara ya utekelezaji wampango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein. (Picha zote na Ikulu)
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
AKITOA maelezo ya Utekelezaji wa Mpangokazi wa Wizara ya Afya katika kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka 2014, Waziri wa Afya Mhe. Rashid Seif Suleiman aliyasema hayo katika mkutano kati ya uongozi wa Wizara hiyo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.
Alisema kuwa katika kipindi cha miezi sita Julai hadi Disemba mwaka jana , Wizara ya Afya imetekeleza mambo mbali mbali hasa katika kuimarisha miundombinu ya afya pamoja na vifaa vya matibabu.
Akitaja miongoni mwa mambo hayo Waziri Suleiman alisema kuwa n i pamoja na kukamilika na kuanza kazi za utoaji wa huduma kwa jengo jipya la upasuaji wa maradhi ya ubongo na uti wa mgongo katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
Jengine ni kuanza kazi za ujenzi wa wodi ya watoto kwa ufadhili wa Norway, kumaliza ujenzi wa ICU mpya kupitia ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China katika hospitali ya Mnazimmoja pamoja na kuanza kwa hospitali ya Abdalla Mzee ya Mkoani Pemba.
Mafanikio mengine ni ununuzi wa mashine ya X-Ray katika hospitali ya Mnazimmoja, kuanza kazi za ujenzi kwa ajili ya utanuzi wa Hospitali ya Micheweni pamoja na ujenzi wa chumba cha upasuaji, kumalizia wodi ya wazazi na watoto pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wete.
Aidha, aliyataja mafanikio mengineyo ni upatikanaji wa Ambalesi 4 aina ya Landcrucer kutoka UNFPA ambazo mbili zitatumika Pemba na mbili zitatumika Unguja, kufanikiwa kwa chanjo ya Rubella kwa asilimia 87 na kupatikana kwa shetria ya Baraza la Wauguzi na wakunga na mengineyo.
Sambamba na mafanikio hayo, Waziri Suleiman alieleza changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na ukarabati wa jengo la kutolea huduma za macho katika hospitali ya Manammoja na ujenzi wa eneo la kusubiria kwa jamaa za wagonjwa wanaofika katika hospitali ya Mnazimmoja.
Pamoja na hayo, Waziri Suleiman alieleza muhtasari wa malengo na mikakati ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha unaoendelea ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundommbinu ya faya, huduma za afya kwa jamii ili kupunguza maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na kuongeza upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendananishi kwa hospitali na vituo vya afya vya Serikali.
Wizara hiyo pia, ina lengo la kutayarisha na kupitia miongozo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za afya, kuanzisha mfumo wa kupimia utekelezaji wa wafanyakazi, kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini katika sekta hiyo na kuendelea na mchakato wa kuanzisha vyanzo mbadala vya upatikanaji wa rasilimali fedha ikiwemo Bima ya Afya.
Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alieleza juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakisha Wizara hiyo inaendelea kupata mafanikio kwa lengo la kutoa huduma stahiki kwa jamii.
Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Wizara hiyo kwa matayarisho mazuri ya utekelezaji wa Mpangokazi wake kwa robo mbili kati ya Julai hadi Disemba 2014 huku akisisitiza kuongeza juhudi ili mafanikio zaidi yaweze kupatikana.
Wakati huo huo, Dk. Shein alifanya mkutano na uongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo uongozi huo ulieleza majukumu ya Wizara hiyo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai hadi Disemba 2014.
Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa Wizara hiyo inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa tija inapatikana kwenye sekta ya uvuvi na mifugo huku akisisitiza haja ya kutumia taaluma, sheria na taratibu katika kutatua mizozo hasa ile ya uvuvi.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Serikali imo katika kuweka misingi ya kuhakikisha wavuvi wanavua bahari kuu sambamba na kutafutiwa vifaa zikiwemo boti za kisasa huku Serikali ikifanya juhudi katika kuimarisha ufugaji wa samaki kwa lengo la kuinua sekta hiyo.
Sambamba na hayo, alisema kuwa jitihada za kinga ziendelee ikiwa ni pamoja na kuwapa wananachi elimu juu ya maradhi yanayotokana na wanyama ili wapate kujikinga.
Mapema Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdilah Jihad Hassan, akitoa taarifa ya Utekelezaji Mpangokazi wa wizara hiyo alisema kuwa miongoni mwa malengo yaliopangwa kutekelezwa kwa mwaka huu wa fedha ni pamoja na kuimarisha huduma za ugani ili ziweze kuwafikia walengwa wote walio katika sekta ya mifugo na uvuvi.
Aidha, alieleza malengo mengine kuwa ni kuendelea na ufugaji wa samamki, uvuvi wa kienyeji na wa kina kirefu, kuongeza uwezo wa watumishi katika nyanja mbali mbali ili waweze kuwahudumia wananchi kwa urahisi zaidi pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa kwa lengo la kuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi.
Pamoja na hayo, Waziri Jihadi alitumia fursa hiyo kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumpongeza Dk. Shein kwa hatua anazozichukua katika kuiongoza nchi kwa busara na hekima kubwa.
“Tunaamini kwamba hekima na busara ulizoendelea kuzitoa itakuwa ani chachu katika kuiletea maendeleo Zanzibar.
Uongozi huo ulieleza kuwa kutokana na miongozo aliyowapa katika kuendeleza sekta ya Uvuvi na Mifugo nchini, wavuvi na wafugaji pamoja na wadau wengine katika sekta hizo wamepata maendeleo makubwa.
Katika mkutano huo, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, nae alihudhuria.
No comments:
Post a Comment