TANGAZO


Thursday, February 12, 2015

Rais Kikwete awaapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Balozi wa Tanzania nchini Kenya

Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua akisaini baada ya kuapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akisaini hati baada ya kumwapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua mara baada ya kumwapisha wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule akisaini baada ya kuapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akisaini hati baada ya kumwapisha Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule mara baada ya kumwapisha wakati wa hafla ya kumwapisha iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule mara kabla ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete  leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule mara kabla ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete  leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi viongozi na watumishi wa Serikali waliohudhuria hafla ya kuwaapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule wakati wa hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule (kulia) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua na familia yake mara baada ya kuapishwa katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimrekebisha tai Aman Mwinyimvua ambaye ni mtoto wa Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara Fedha mara baada hafla ya kumwapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule leo Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Na Eleuteri Mangi –MAELEZO
12/02/2015
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amewaapisha Dkt. Hamisi Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Balozi wa Tanzania nchini Kenya John Haule katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia nafasi yake ya sasa, Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua amemshukuru Rais kwa kumteua ili akaongeze nguvu katika Wizara ya Fedha kwa kuwa yeye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi.

“Naenda kuwa sehemu ya viongozi wa wizara, hivyo naenda kuungana na timu ya viongozi waliopo ili niweze kuchangia kukuza uchumi wa nchi yetu” alisema Dkt. Mwinyimvua.

 Dkt. Mwinyimvua amesema kuwa atashirikiana na viongozi waliopo katika wizara ya Fedha ikizingatiwa wapo Waziri, Manaibu Waziri, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na watumishi wa Wizara nzima.

Aidha, Balozi Haule amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Hafla hiyo ilihudhriwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe, viongozi na watumishi mbalimbali wa Serikali.

No comments:

Post a Comment