Mahakimu na Wanasheria wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha siku ya Sheria Zanzibar sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kushoto) alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar katika kilele cha siku ya Sheria Zanzibar(katikati)Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Jaji Mkuu wa Mahakama kuu Tanzania Shaaban Ally Lila (kushoto) alipowasili katika viwanja vyaVictoria Garden Mjini Zanzibar katika kilele cha siku ya Sheria Zanzibar(katikati) Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akifuatiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abibakar Khamis Bakary wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu alipokuwa akisema machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ali azungumze na Wananchi, Mahakimu na Wanasheria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu baada ya kikizindua kitabu cha Mwaka wa Sheria leo katika Sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Mwaka wa Sheria kama ishara ya uzinduzi wa kitabu hicho samba samba na maadhimishoya siku ya Sheria Zanzibar(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na wapili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Sheria sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande(kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
JUHUDI zinazofanywa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kielelezo thabiti cha kuhakikisha Mahakama
zinaendelea kuwa huru, zinafuata misingi ya utawala bora na zinakwenda sambamba
na mabadiliko ya teknolojia, kiuchumi na kijamii yanayoendelea kutokea ndani na
nje ya nchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye maadhimisho ya siku ya
Sheria Zanzibar huko katika viwanja vya Victoria Garden, mjini Zanzibar.
Dk. Shein alisema kuwa mafanikio yanayoendelea kupatikana katika kukuza
demokrasia na uatawala bora nchini ni matunda ya juhudi na mashirikiano ya
pamoja, hivyo ipo haja ya kuongeza kasi katika kuhakikisha mahkama zinaendeshwa
kwa njia za kisasa zinazopelekea kuwepo kwa ufanisi na kuondosha mrundikano wa
kesi.
kwa lengo la kuongeza ufanisi katika sekta ya Sheria, Serikali imeandaa
Mkakati wa Mabadiliko katika Sekta ya Sheria Zanzibar (2014-2019) unaotekelezwa
na taasisi mbali mbali zilizo ndani na nje ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Alisema kuwa miongoni mwa malengo ya Serikali katika utekelezaji wa Mkakati
huo ni pamoja na kuimarisha mfumo wa haki za jinai ambao utahakikisha usalama
na amani kwa wananchi, kuimarisha mfumo wa haki za madai na kuongeza ufanisi
katika kuongeza uwezo wa kupata haki na huduma za kisheria.
Aidha, Dk. Shein alitoa Wito kwa Taasisi za Serikali na zisizo za
Kiserikali zikiwemo Jumuiya ya Wanasheria Zanzibar (ZLS), Chama cha Wanasheria
Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC),
kutekeleza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa.
Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Jaji Mkuu wa Zanzibar
pamoja na viongozi wenziwe wa Mahkama kwa uamuzi wao wa kujiunga na Jumuiya ya
Mahakimu na Majaji ya Afrika Mashariki ikiwa ni mwanachama wa kushirikishwa.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alitoa wito wa kuongezwa kwa kasi ya kuanzishwa
kwa Mahkama ya Biashara ili kuimarisha sekta ya biashara ambayo ni muhimu kwa
ustawi wa jamii na maendeleo.
Katika hotuba hiyo, Dk. Shein alisema kuwa Majaji, Mahakimu na Wanasheria
wana jukumu kubwa katika kuifanikisha kampeni ya unyanyasaji wa kijisia kwani
bado kuna changamoto kubwa katika kutimiza matarajio ya wananchi hasa katika
uendeshaji wa kesi za udhalilishaji ambapo zipo lawama na malalamiko kutoka kwa
wananchi juu ya usimamizi na uendeshaji wake.
Dk. Shein alieleza kuwa serikali inalifanyia kazi suala la kuanzishwa kwa
Mfuko wa Mahakama pamoja na Baraza la Wawakilishi utaratibu ambao utasaidia kutoa uhuru katika
mihimili hiyo.
Katika sherehe hizo, Dk. Shein pia, alizindua kitabu cha mwaka.
Naye Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis Bakar, alisema kuwa maana
halisi ya uhuru wa Mahakama kuwa msingi wa utawala bora ni kuwa na nguvu, uwezo
na uhuru wa Mahakama katika kuwatumikiwa watu ambalo hilo ndio lengo la kaauli
mbiu ya mwaka huu.
Alisema kuwa kuwaweka wananchi mwanzo na kuwatumikia kwa kupitia nguvu za
Mahakama ndio kiini cha autendaaji wa Mahakama za hapa Zanzibar.
Alisisitiza kuwa katika miongo hii ya utandawazi na hali ya uchumi ni
lazima Mahakama za hapa nchini zibadilike na zijikite katika kuwatumikia watu
vizuri kwa mujibu wa taratibu zilkizowekwa ambao huo ndio utoaji wa haki ulio
huru kwa kuleta utawala bora.
Pamoja na hayo, alieleza kuwa bado tatizo lakutokomeza unyanyasaji wa
kijinsia haalijafanikiwa vizuri hapa nchini kwani wazee na jamaii ni wagumu
sana wa kutoa msaada wao na mashirikiano yao na vyombo vya sheria.
Nae Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu alisema kuwa kauli mbiu ya siku ya sheria mwaka huu ni ‘
Mahkama huru msingi wa utawala bora’, hiyo ni kutokana na kuzingatia kuwa mwaka
huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa tokea kushika madaraka ya kuongoza nchi Dk. Shein amekuwa
akichukua jitihada mbali mbali yeye binafsi pamoja na serikali anayoiongoza
katika kuweka na kusimamia vyema misingi ya utawala bora.
Jaji Makungu alisema kuwa kuwepo kwa Mahkama huru ni moja ya misingi ya
utawala bora kwani kukosekana kwa mahkama iliyo huru na inayotoa haki kw
wananchi tena kwa wakati inaweza kupelekea kukosekana kwa amani na utulivu
katika nchi.
Sambamba na hayo, Jaji Makungu alimuhakikishia Dk. Shein kuwa Mahkama
itajipanga vizuri kukabiliana na hali itakayojitokeza ya masuala ya uchaguzi na
itahakikisha kuwa Mahakimu wanatenda haki kwa mujibu wa viapo walivyokula na
hawajiingizi katika ushabiki wa kisiasa wakati wa kushughulikia rufaa za
uandikishaji.
Aidha, alisema kuwa watahakikisha Mahakimu wanabaki katika ili kujaza fomu
za wagombea wakati ukifika na kusisitiza kuwa endapo malalamiko ya uchaguzi
yatafunguliwa na wagombea Ubunge au Uwakilishi na Udiwani, basi watashughulikia
haraka ipasavyo.
Nae Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan alisema kuwa dhana ya Uhuru wa Mahakama ni kigezo muhimu katika
kupima Utawala Bora na ni dhana inayopingana na dhana ya kwamba 'Mtawala
hafanyi makosa' kwani katika dhana hiyo mtawala anaaminika mkuu kuliko sheria.
Lakini kutokana na Mapinduzi ya masuala ya kijamii kwa mujibu wa
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar dhana hii imekuwa haina nafasi hasa katika ukuaji
wa demokrasia baada ya kuondoshwa kabisa kwa dhana ya utawala wa kibabe.
Alisema kuwa dhan ya Utawala bora ni dhana pana inayojumuisha uwazi, uwajibikaji,
ushiruikishwaji wa watu, ufanisi, tija uadilifu, usawa na kuheshimu utawala wa
sheria.
Alisisitiza kuwa utoaji wa haki unapokuwa hauna uadilifu, haufuati msingi
wa usawa na utawala wa shreia unaweza ukabadilisha hata uvunjifu wa amani.
Alisema kuwa rushwa haina maana
kwamba Jaji au Hakimu amepokea akiasi fulani cha fedha bali ametoa hukumu
isiyokuwa na misingi ya haki na utawala wa sheria au maadili mazima ya kazi
yake hakuyafuata.
"Ni wajibu wetu sisi sote wenye dhamana ya kusimamia Sheria kuhakikisha
kwamba tunaisaidia Mahakama katika kutimiza wajibu wake wa kutoa
haki"alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Nae Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Ibrahim Mzee alisema kuwa uhuru wa Mahakama si
zawadi bali ni msingi wa Kikatiba na ni msingi wa Utawala Bora unaoandamana na
jukumu kubwa la Mahakama katika kazi ya utoaji wa haki.
Alisema kuwa dhana ya Utawala Bora inasisitiza kwamba jitihada za kuleta na
kuendeleza usalama na maendeleo katika nchi ni lazima ziwe za kidemokrasia na
zizingatie haki za binaadamu, uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji, uadulifu,
ufanisi na utawala wa sheria.
Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar Awadh Ali Said nae alisema kuwa
wakati umefika wa kuaznishwa kwa Mfuko wa Mhimili wa Mahakama ambao utatumika
kwa ajili ya kugharamia shughuli za utawala, uendeshaji na maendeleo ya Mhimili
wa Mahkama.
Alisisitiza kuwa iwe jukumu la Serikali katika kuhakikisha kwamba katika
kila bajeti ya mwaka husika, inatenga kiwango kinachotosha cha fedha ambazo
zitaingizwa katika Mfuko wa Mhimili wa Mahakama.
Aidha, alisema kuwa ipo haja kwa Serikali na Taasisi zenye jukumu la
kupambana na rushwa pamoja na wadau wote wa sheria kushirikamana na kuondoa
kilio hicho cha wananchi ili kurudisha imani na heshima yao kwa chombo hicho.
Viongozi mbali mbali walihudhuria katika hafla hiyo, akiwemo Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed
Othman Chande, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila, Naibu
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Abdalla Ali, Majai wa Mahkama Kuu, Msajili
Mkkuu wa Mhkama ya Tanzania, Mahakimu na Makadhi pamoja na viongozi wa dini na
serikali na wananachi mbali mbali.
No comments:
Post a Comment