Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ikilu jana jijini Dar es salaam akiwa na mgeni wake Rais wa Ujerumani Rais wa Ujerumani Joachim Gauck (kushoto). Rais Gauck yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwa siku tano.
(Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
04/02/2015
TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazosimamia uhuru habari na inaongoza kwa kuwa wa vyombo vingi habari yakiwemo magazeti.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua sababu za kusimamisha uingizaji nchini gazeti la “The East African”, wakati wa mkutano wa waandishi wa habari yeye na Rais wa Ujerumani Joachim Gauck.
Rais Kikwete alisema kuwa gazeti hilo halikufuata utaratibu wa kusambazwa nchini kulingana na sheria na taratibu za nchi, hata hivyo Serikali imeshawasiliana na wahusika na wameelekezwa utaratibu wa kufuata kulingana na sheria za nchi.
“Tanzania injali na kusimamia uhuru wa habari, kuna magazeti mengi yakiwemo ya kila siku, wiki ambayo yanayomilikiwa na makampuni binafsi ikilinganishwa na magazeti yanayomilikiwa na Serikali” alisema Rais Kikwete
Rais kikwete aliyataja magazeti yanayomilikiwa na Serikali kuwa ni pamoja na Daily News na Habari Leo ikilinganishwa na magazeti yanayomilikiwa na makampuni binafsi ambapo aliyataja magazeti hayo kuwa ni The Guardian, The Citizen, Majira, Mwananchi, Nipashe na mengine mengi.
Rais wa Ujerumani na msafara wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambayo ni mwaliko walioupata kutoka kwa Dkt. Kikwete alipotembelea Ujerumani hivi karibuni na kutunukiwa tuzo ya kufanya vizuri katika suala la chanjo kwa watoto.
Ugeni huo wa Rais Gauck watapata fursa ya kujionea maeneo mengi yenye vivutio vya watalii nchini yakiwemo Visiwa vya Zanzibar na Arusha ambayo yanajulikana kwa utajiri wa vivutio hivyo barani Afrika na duniani.
Ujio wa Rais Gauck nchini na msafara wake unafuatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo mbili wa muda mrefu kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi wao kiuchumi, kisiasa na kijamii.
No comments:
Post a Comment