Shirika lijihusishalo na maswala ya usalama na ushirikiano barani Ulaya,OSCE limesema hali ya Mashariki ya Ukraine inazidi kuwa mbaya na mashambulizi dhidi ya Raia yanazidi kuongezeka.
Msemaji wa OSCE,Shirika linafuatilia hali ilivyo nchini Ukraine amesema silaha zilizopigwa marufku kimataifa zilitumika juma lililopta katika mji unaoshikiliwa na waasi Luhansk.
Amesema mabomu ambayo yalipigwa marufuku kutumika kwenye maeneo ya Watu wengi chini ya Sheria za kimataifa yamesababisha madhara kwa Raia na kuharibu mali zao.
Baadae hii leo, Mkuu wa Shirika la OSCE atahutubia Baraza lake la kudumu, anatarajiwa kutoa wito wa kusitisha mapigano kwa muda katika Mji unaodhibitiwa na Serikali wa Debaltseve ambao mapigano yameongezeka Wiki za hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment