TANGAZO


Tuesday, February 3, 2015

BUNGENI LEO MJINI DODOMA

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandishi Athumani Mfutakamba akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMasuala ya Ukimwi Lediana Mng'ong'o akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni waliofika kwenye Bunge la Jamhuri wakifuatilia Bunge.
Baadhi ya wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma akiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Dkt. Lucy Nkya (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe. Kapt (Mstaafu) George Mkuchika (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge kwenye mlango wa Bunge mjini Dodoma. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma)

Serikali yaingia mkataba wa shilingi bilioni  1 na Serikali ya Japan
  
Na Lorietha Laurence – Maelezo Dodoma
SERIKALI imeingia mkataba wa shilingi Bilioni  1 na Serikali ya Japan  kwa lengo la kutoa mkopo wa masharti nafuu kwa wajasiriamali wadogo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo alipohoji kuhusu mpango wa serikali  kuanzisha kiwanda cha kusindika matunda katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa  mpaka sasa wizara yake kupitia SIDO imeweza kutoa mafunzo  ya usindikaji kwa wajasiriamali wadogo ili kuwajengea uwezo  wa kuanzisha viwanda vidogo vya usindikaji matunda kwa utaratibu wa programu ya Muunganisho  Ujasiriamali vijijini (MUVI).

“Mkakati wa serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mazao ya kilimo yakiwemo matunda yanaongezeka thamani kabla ya kuuzwa” alisema Waziri Kigoda.

Alibainisha kuwa Serikali, imekuwa  ikihamasisha sekta binafsi  kuwekeza  katika ujenzi wa viwanda katika maeneo ambayo malighafi ya kutosha inapatikana ikiwemo ile ya uzalishaji wa matunda.

Aidha alishauri kuwa wakulima wa wilaya ya Kisarawe wauze matunda yao kwenye kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa mpaka pale serikali itakapopata   mwekezaji wa kujenga kiwanda  hicho.

Naye mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari alihoji kuhusu walengwa wa fedha za fidia kwa eneo lilitengwa kwa ajili ya mradi wa EPZ kwa wananchi wa Malula.


Waziri Kigoda alieleza kuwa   jumla ya ekari 4000 zilibainishwa  na oradha ya  wananchi waliopisha mradi huo inashughulikiwa na Halmashauri ya Arumeru.


Nkamia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari  kuwakatia Bima wafanyakazi wao

Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma
NAIBU Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari  kuwakatia wafanyakazi wao bima ili ziweze uwasaidia wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini.
Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac,  kuhusu mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya kazi katika matukio hatari, Naibu Waziri  Nkamia alisema kuwa serikali  inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na inawajibika kikatiba katika kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo wanahabari.

 “Uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma  nyingine muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na ni muhimu kufahamu  na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa katika eneo la kazi”alisema Nkamia.

Aidha alibainisha kuwa  jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari ni kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao ya kazi na pia kuzingatia  miiko ya taaluma yao kwa kuangalia wanayotakiwa kufanya na kutofanya katika eneo husika.

Aliongeza kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila shuruti kwa kuwa nao ni wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna aliye juu ya sheria.
 .
Hata hivyo Serikali  imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa maalum katika matukio mbalimbali ya kitaifa  ikiwemo vitambulisho na mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote.
Naibu Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa ikiandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa mbugeni wakati wowote kuanza sasa.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akijibu hoja za kamati na wabunge mjini Dodoma. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijibu hoja Bungeni kuhusu wizara yake. 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akijibu hoja za kamati hoja za kamati.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Said Nkumba akiwasilisha taarifa ya kamati yake. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma)


Waziri Lukuvi atangaza mapambano dhidi ya wanaodhulumu ardhi

Na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali itahakikisha inapambana na watu wote wanaoendesha vitendo vya dhuluma, matapeli na wanaonyang’anya viwanja, majengo, mashamba na ardhi za wanyonge.

Waziri Lukuvi ametangaza azma hiyo wakati akijibu baadhi ya hoja za wabunge waliochangia Taarifa ya Kamati ya Bunge, ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyowasilishwa na kupitishwa Bungeni mjini Dodoma.
Alisema anatambua kwamba hasa maeneo ya mijini kuna dhuluma nyingi zinafanyika ambapo masikini, mayatima na wajane wanadhulumiwa  na kunyang’anywa ardhi na majengo yao.

“Wizara yangu tutahakikisha tunapambana sana na watu wote, wakubwa na wadogo, matajiri na watumishi wa Serikali waisio waaminifu na matapeli wote wanaoendesha vitendo vya dhuluma na kunyang’anya viwanja, majengo, mashamba na ardhi za wanyonge” alisema Lukuvi.

Aliongeza “Najua mijini hasa kuna dhuluma nyingi, masikini hasa wanadhulumiwa, mayatima na wajane wananyang’anywa ardhi na majengo yao.Tunajua baadhi ya wafanyakazi wa ardhi wasio waaminifu wanashirikiana”.

Alisema moja ya kazi kubwa ya Wizara yake ni kuhakikisha kwamba wanashirikiana ili kuhakikisha wanatokomeza udhalimu huo unaoendelea nchini.
Kwa upande wa migogoro ya ardhi ambayo inaripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini, Waziri Lukuvu alisema watashirikiana na Wizara husika na wananchi kwa ujumla ili kuitatua.

“Lakini pia tutashirikiana na wananchi, Wizara ya Maliasili na TAMISEMI.Tutakaa pamoja kuhakikisha tunasuluhisha hii migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali yanayohusu miji na yanayohusu vijiji” alisema Waziri Lukuvi.

Alibainisha kwamba migogoro ni mingi na wanaosababisha migogoro hiyo ni watu, kwa hiyo ameomba ushirikiano na taasisi na watu mbalimbali kumaliza migogoro hiyo.

Alisema badala ya wananchi kwenda Dar es Salaam kushughulikia migogoro yao, yeye pamoja na watendaji wa wizara watatembelea mikoani ili kutatua migogoro hiyo.

“Na mimi nimeamua sasa badala ya watu kuja Dar es Salaam kumfuata Waziri na makamishna, sasa mimi nitapanga ratiba nitakuja huko kila mkoa na watalamu wote muhimu wenye uwezo wa kuamua”alisema na kuongeza:

“Ili tuje tutatue migogoro huko huko kwenye maeneo.Ile ambayo ipo kwenye uwezo tutaitatua palepale, ile ambayo itahitaji kuitolea majibu mafupi tutaitolea majibu, tunaombeni ushirikiano wenu”.
Waziri Lukuvi alijibu hoja ya Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah aliuliza hatma ya shamba la Utumaini la Mafia, na kusema Serikali imechukua hatua na imetoa notice ikiwa ni hatua za kulichukua  shamba hilo lenyewe ukubwa wa hekari 1000.

“Tayari tumeshatuma kwa anayejifanya anamiliki hilo shamba tarehe 28 mwezi huu notice ya kutaka kulichukua hilo shamba ambalo tutasubiri muda wa siku 90 zikiisha hatua zinazofuata zitaendelea” alisema.
Hivyo alimtaka mbunge Shah na wananchi wa Mafia watambue kwamba Serikali imeshaanza kuchukua hatua juu ya shamba hilo na mengine ambapo alibainisha kuwa lengo la Serikali ni kulichukua shamba lote.

Akiwasilisha Taarifa ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati James Lembeli ,alitaja migogoro mbalimbali ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini huku akiishauri Serikali kuimaliza migogoro hiyo.

No comments:

Post a Comment