Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi na Mbunge wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kapteni Mstaafu John Chiligati, akichangia hoja.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Sabrina Sungura aichangia hoja.
Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman akichangia taarifa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage, akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) baada ya Bunge kuvunjwa.Katikati ni Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akibadilishana mawazo na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata.
Baadhi ya wafugaji waliohudhuria
Bungeni wakizaungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuvunjwa
kwa Bunge.
Waziri Mkuu Pinda awaambia wakulima, wafugaji wanahaki ya kuishi popote
Na
Lorietha Laurence-Maelezo, Dodoma
WAZIRI Mkuu Mizengo
Pinda ametoa rai kwa wakulima na wafugaji nchini kujikubali kuwa wote ni Watanzania na wanahaki
ya kuishi popote bila kuvunja sheria.
Amesema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akipokea
na kukubali taarifa na mapendekezo iliyotolewa na kamati teule ya Bunge ya
kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi,kilimo,mifugo,maji
na uwekezaji.
“Nimepokea mapendekezo
yote yaliyotolewa na kamati na ninaahidi yatafanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi
wa Tanzania” alisema Pinda.
Aliongeza kuwa kwa
utekelezaji wa awali serikali itauunda tume maalum ya wataalum mchanganyiko na tume ya makatibu wakuu ili kuweza kupitia taarifa hizo
na baadaye kuwasilisha kwa ajili
ya utekelezaji.
Aidha alisema ni wajibu wa Wizara ya Ardhi
kupima ardhi katika maeneo mbalimbali na
kwa wale wanaokiuka taratibu wachukuliwe
hatua madhubuti ya kuwawajibisha.
Hata hivyo Waziri Pinda
alisema kuwa kuna umuhimu wa kutolewa
kwa elimu ya kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuitunza amani ya nchi
yetu katika kuleta mabadiliko na kuondokana na mgawanyiko.
Vile vile alizitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwachunguza watendaji wake
wanaokiuka sheria na taratibu za utendaji na baadaye kuweza kuwawajibisha.
Naye Mwenyekiti wa
kamati hiyo teule Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alisema kuna haja
ya kuwatengea maeneo yaliyopimwa wafugaji na wakulima ili kuepusha vurugu kwa jamii hizo mbili.
“Naiomba serikali iweze
kushughulikia suali hili la wafugaji na wakulima ili kuepukana na migogoro
inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo” alisema Ole Sendeka.
Tanzania ina chakula cha ziada
Na Hussein
Makame-MAELEZO, Dodoma
TANZANIA ina
ziada ya tani Milioni 3.2 za chakula kutokana na uzalishaji wa mazao ya chakula
katika msimu wa 2013/2014 kufikia jumla ya tani Milioni 16.0 wakati makadirio
ya mahitaji ya chakula kwa mwaka 2014/2015 ni tani Milioni 12.8.
Hayo
yamesemwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akisoma hotuba ya kuahirisha
mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliokaa kwa siku 12
mjini Dodoma.
“Tathmini ya
awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini hadi Mwezi Septemba mwaka 2014
inaonesha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa kilimo 2013/2014
ulifikia jumla ya Tani Milioni 16.0 zikiwemo Tani Milioni 9.8 za mazao ya
nafaka na Tani Milioni 6.2 za mazao yasiyo ya nafaka” alisema Waziri Mkuu
Mizengo Pinda.
Alisema
kutokana na hali hiyo, Tanzania imeweza kujitosheelza kwa chakula kwa asilimia
125, hali iliyomfanya kuwapongeza wakulima kwa kuitikia wito wa Serikali wa
Mpango wa Kilimo Kwanza ambao umeongeza tija katika uzalishaji.
Kwa upande
wa utekelezaji wa maagizoya ujenzi wa maabara nchini, Waziri Mkuu Pinda
aliwataka wakuu wa mikoa, wilaya, mameya, wenyeviti na wakurugenzi watendaji wa
halmashauri za wialaya na miji nchini kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa.
Alisema hadi
kufikia Desemba mwaka jana, mkoa wa Njombe ambao ulifanikiwa kukamilisha ujenzi
wa vyumba vya maabara kwa asilimia 96 ya shule za sekondari zilizopo mkoani
humo huku mkoa wa Ruvuma na Morogoro ukikamilisha ujenzi huo kwa asilimia 81,
53 mtawalia.
Aliitaka
mikoa ambayo haijakamilisha ujenzi huo kuhakikisha inakamiliasha hadi kufikia
mwezi Juni, 2015 kama Rais Jakaya Kikwete alivyoagiza.
Akizungumzia
utekelezaji wa Mradi wa REA wa upatikanaji wa nishati ya umeme vijijini, Waziri
Mkuu alisema idadi ya Watanzania waliounganishwia umeme imeongezeka kutoka
asilimia 2.5 kwa mwaka 2007 hadi asilimia 18.4 kwa mwaka 2010 na kufikia
asilimia 24 kwa mwaka 2014.
Katika
Mkutano huo wa 18 wa Bunge la Jamhuri, jumla ya maswali 122 ya msingi na 313 ya
ngongeza yaliulizwa na wabunge na maswali 15 ya msingi kwa Waziri Mkuu na
nyongeza 13 yaliulizwa.
Mkutano huo
umeahirishwa hadi Machi 17 mwaka huu ambapo Bunge hilo litakutana tena katika
Mkutano wa 19.
No comments:
Post a Comment