Mshambuliaji wa timu ya Yanga Kpah Sharman kulia na beki wa timu ya JKU Pansiano Malik wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa robo fainali ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Andrey Coutinho, akipiga mpira golini kwa timu ya JKU, katika mchezo wao wa robo fainali uliofanyika uwanja wa Amaan.
Beki wa timu ya JKU, Issa Khaidary,akiondoa mpira huku mshambuliaji wa timu ya Coutinh, akijaribu kunyanganya mpiwa wakati wa mchezo wao wa robo fainali ya kombe la mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan. timu ya JKU imeshinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Kpah Sharman, akimpita beki wa timu ya JKU, Issa Khaidary. ikiwa wanawania kuingia Nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya JKU imefanikiwa kuingia nusu fainal baada ya kuifunga Yanga bao 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Sharman akimpita beki wa timu ya JKU katika mchezo wao wa Robo fainali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya JKU imeshinda 1-0.
Mchezaji wa timu ya JKU Abdllah Waziri akimpita beki wa timu ya Yanga Oscar Joshua.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Saimon Msuva akiruka kjiunzi cha beki wa timu ya JKU akiwa chini.
Mmiliki wa Blog ya BinZubery (kulia), akisisitiza jambo na Mwandisha wa gazeti la nipashe Sanula Athanas, wakati wa mchezo wa Yanga na JKU uliofanyika uwanja wa Amaan.
Golikipa wa timu ya JKU Mohammed Abdurahaman, akidaka mpira huku mshambuliaji wa timu ya Yanga Saimon Msuva akiwa jirani akinusa mpira huo.
Golikipa Mohammed Abdurahaman wa JKU.
Wachezaji wa timu ya JKU wakiingia uwajani baada ya kumalizika dakika 15 za mapumziko wakati wa mchezo huo dhidi ya Yanga wa kuwania kucheza Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Aman, mjini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya JKU wakishangilia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga wakati wa mchezo wao wa kuwania kucheza Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Aman, mjini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Kocha wa timu ya JKU akizungumza na waandishi wa habari baada ya timu yake kuitoa Yanga kwa kuifunga bao 1-0 na kutinga hatua ya Nusu Fainali. Kocha wa Yanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo kumalizika wakilala kwa bao 1-0 mbele ya JKU katika mchezo wa kuwania kucheza Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Aman, mjini Unguja usiku wa kuamkia leo. Wachezaji na mashabiki wa timu ya JKU wakishangilia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga wakati wa mchezo wao wa kuwania kucheza Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Aman, mjini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya JKU wakishangilia ushindi huo wa bao 1-0 dhidi ya Yanga. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews Blog)

No comments:
Post a Comment