Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wakiwa wameanza ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Sehemu ya maungio ya mradi wa bomba jipya kutoka mtambo wa Ruvu Chini yaliyopo eneo la Mpiji wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kukagua mabomba yaliyohifadhiwa eneo la Kibaha Mwendapole wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Meneja wa Mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu Pintu Dutta kwa kampuni ya VA TECH WABAG kutoka India akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) walipotembelea huo eneo la upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi
ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA)
wakitembelea sehemu unapofanyika upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu wakati wa ziara
yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kukagua na kujionea
hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu
Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi
katika mikoa hiyo.
Moja ya hatua ya
kusafisha maji katika mtambo wa Ruvu Juu kabla ya kusafirishwa tayari kwa
matumizi kwa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
WAJUMBE wa Kamati ya Ufundi
ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wamefanya
ziara ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea
hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu
Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi
katika mikoa hiyo.
Ziara ya wajumbe hao wa
kamati Ufundi ilianza kwa kukagua kazi ya ukarabati wa kituo yalipo matangi ya
maji eneo la Chuo Kiukuu cha Dar es salaam, maungio ya mradi wa bomba jipya
yaliyopo eneo la Mpiji, ujenzi wa ofisi ya mradi wa bomba kuu la maji kutoka
Ruvu Juu zilizopo Kibaha, kukagua mabomba yaliyohifadhiwa eneo la Kibaha
Mwendapole na upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu Mladizi na Ruvu darajani.
Akifanya majumuisho ya
ziara hiyo Mwenyekiti wa wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya DAWASA Christine
Kilindu amesema kuwa wajumbe wameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miundo mbimu
hiyo ambapo matarajio mradi huo utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa mwishoni
mwa mwaka huu.
Mwenyekiti huyo
alisisitiza kuwa wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani watarajie kupata
huduma ya maji iliyo bora mara miradi ya Ruvu Juu Chini itakapokamilika.
Aidha, Christine
amewaasa wananchi wa maeneo yanapopita mabomba wa miradi hiyo kuyatunza vizuri
kuanzia wakati huu yalipohifadhiwa na yatakapokuwa yameanza kutumika ili
yawanufaishe wananchi wote wa mikoa hiyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi
DAWASA Romanus Mwang’ingo alisema kuwa pamoja na kuboresha huduma kwa maeneo
yaliyo pembezoni mwa barabara ya Morogoro yaani Kimara, Mbezi, Kiluvya, Kibaha,
Visiga, Mlandizi na Kibamba, utekelezaji huo pia utawanufaisha wakazi wa Ubungo,
Vingunguti, Kimara, Tabata na Kinyerezi ambao nao wanahudumiwa na mtambo
unaotoa maji kutoka Ruvu Juu.
Mradi wa upanuzi wa mtambo
wa Ruvu Chini unalenga kuongeza uzalishaji maji na kuwahudumia wakazi wa maeneo
ya uwekezaji (EPZ), Chasimba, Buma, Zinga, Kerege, Mpiji, Bunju, Wazo,
Salasala, Madale, Kinzudi, Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani,
Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni,
Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala.
Kazi hiyo ya maboresho
inafanyika chini ya mpango maalumu wa kuboresha huduma ya upatikanaji wa Maji
Safi na Maji Taka jijini Dar es salaam na maeneo mengine yanayohudumiwa na
DAWASA unaohususha ujenzi wa miradi mipya na pamoja na kukarabati miundombinu
iliyopo.















No comments:
Post a Comment