Wananchi wakifuatilia ziara
ya kushtukiza ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum aliyofanya leo jijini Dar es
salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia
na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa
kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na
kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
NA Eleuteri Mangi-
MAELEZO
22/01/2015
Uelimishwaji bado
unahitajika kwa wafanya biashara nchini katika na kuhakikisha wazingatia na
kusimamia matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za EFD.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipofanya ziara
ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia
na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa
kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na
kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini.
“Nasisitiza
wafanyabiashara wote nchini kutumia
mashine za kielektroniki za EFD katika biashara zao, niwaombe muwe na mwamko wa
ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi yetu ” alisema Waziri Saada.
Zaidi nya hayo, Waziri
amesisitiza kuwa wafanyabiashara wajisajili katika mfumo wa VAT ili kuokoa
mapato yanayopotea ambapo ameeleza kuwa nchi zilizoendelea wanatoa misaada kwa
nchi zinazoendelea kutokana na makusanyo ya wananchi wa nchi hizo kujali na
kuthamini kulipa kodi kutoka wafanyabiashara na watumishi wengine.
Pia Waziri Saada
aliuagiza uongozi wa TRA kuwa karibu na wafanyabiashara kwa naq kutoa namba zao
za simu ili wateja waweze kuwasiliana nao mara mashine zao zinapokuwa na
hitilafu na kutoa taarifa kwa haraka badala na kuwa na ufanisi wa haraka nan
wenye tija kwa taifa.
Naye Kaimu Meneja wa
mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Elias Balongo
amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi wote kutambua umuhimu wa
kudai risiti baada ya kununua bidhaa na kwa wafanyabiashsra kutoa risiti baada
ya kuuza bidhaa.
Kwa upande wake
mfanyabiashara wa Namanga jijini Dar es salaam Saleh Kassim Seif alisema kuwa wanaishukuru
Serikali kuanzisha mfumo wa matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD kwani
unamanufaa kwao ambapo unawasaidia kujua mauzo yao ya siku, wiki, mwezi hadi
mwaka ili ambapo wameweza kuboresha bishara zao kwa kuwa na kumbukumbu sahihi
ya mauzo yao.
Aidha, mfanyabiashara
huyo alisema kuwa wanapata changamoto ya
mashine hizo kuharibika wanaomba zitengenezwe ndani ya saa 24 ili waweze kutoa
huduma yenye kuzingatia sheria, kanuni na taraibu za buiashara nchini.
Katika ziara hiyo,
Waziri wa Fedha aliandamana viongozi wa wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA,
waandishi wa habari na baadhi ya maafisa wa saerikali.
No comments:
Post a Comment