TANGAZO


Monday, January 19, 2015

Wateja wa Airtel washauriwa kulipa ada za magari kupitia huduma ya Airtel Money

*Huduma hii inaongeza ufanisi wa ukusanyaji Kodi na kuleta urasihi , usalama na uhakika kwa wamiliki wa magari

Meneja  wa Airtel Money Bw. Asupya Nalingigwa akielezea kuhusu namna ya kulipia ada za magari kupitia huduma ya Airtel Money, huduma inayowawezesha Watanzania kufanya malipo mbalimbali ya TRA kupitia simu zao za mkononi mahali popote nchini.
Meneja  wa Airtel Money Bw. Asupya Nalingigwa akielezea kuhusu namna ya kulipia ada za magari kupitia huduma ya Airtel Money, huduma inayowawezesha Watanzania kufanya malipo mbalimbali ya TRA kupitia simu zao za mkononi mahali popote nchini.
Meneja  wa Airtel Money Bw. Asupya Nalingigwa akionesha kipeperushi kinachoelekeza jinsi ya kulipia ada za magari kupitia huduma ya Airtel Money, huduma inayowawezesha Watanzania kufanya malipo mbalimbali ya TRA kupitia simu zao za mkononi mahali popote nchini.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imewashauri watanzania na wateja  kulipia kodi ya magari kwa mwaka huu kupitia huduma ya Airtel Money, huduma inayopatikana kupitia simu zao za mkononi  mahali popote nchini.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja  wa Airtel Money Bwana Asupya Nalingigwa alisema” Tunatambua sasa mwaka umeanza na magari mengi yatahitaji kulipiwa kodi kwa mwaka huu,  nachukua nafasi hii kuwakumbusha watanzania kwamba wanaweza kulipia kodi zao za magari wakiwa mahali popote  kupitia huduma yetu ya Airtel Money.
Ushirikiano huu kati ya TRA na Airtel unawawezesha watanzania kulipa kodi zao kupitia simu zao za mkononi na kuondoa usumbufu na msongamano uliokuwepo hapo awali. Kwa sasa kupitia huduma ya Airtel Money TRA Magari tumewawezesha watanzania kufanya malipo wakiwa majumbani kwao na sehemu zao za kazi lakini pia tumewawezesha TRA kuongeza makusanyo ya kodi kwa kiwango kikubwa”
Bw, Nalingigwa alifafanua zaidi jinsi ya kufanya malipo hayo na kusema” Ili kufanya malipo mteja anatakiwa awe na kumbukumbu namba (reference number) na kujua kiasi cha ada.
Ili kujua kiasi cha ada ya malipo mteja anatakiwa kutuma ujumbe wenye neno “Assess” na kuacha nafasi kisha kuingiza namba ya gari na kutuma kwenda kwenye namba 15341
Na ili kupata kumbukumbu namba (reference namba)  mteja anatakiwa kutuma ujumbe wenye neno Register kisha kuacha nafasi na kuandika namba ya GARI kisha kutuma kwenye namba 15341.
Baada ya hapo sasa mteja anaweza kuanza kufanya malipo kwa kutumia huduma ya Airtel Money kwa kupiga *150*60# chagua lugha , kisha bonyesha kufanya malipo, kisha chagua TRA MAGARI, ingiza kiasi cha Malipo, hakiki kiasi cha malipo, kisha weka namba ya siri ingiza kumbukumbu namba kisha utapokea ujumbe unaohakiki malipo yako kutoka TRA.
Huduma hii ni kwa wateja wote wa Airtel hivyo tunatoa wito kwa wale wote wanaomiliki vyombo vya moto kutumia fulsa hii kufanya malipo ya ada zao za magari kwa mwaka huu kupitia huduma ya Airtel Money- TRA Magari inayopatikana wakati wote , mahali popote nchini. Aliongeza Nalingigwa

No comments:

Post a Comment