TANGAZO


Sunday, January 18, 2015

Watano wajishindia fedha promosheni ya Jaymillions

*Kila mmoja ajishindia kitita cha shilingi milioni 1
Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao aliyesimama(kushoto)akionyeshwa namba ya mmoja wa washindi na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)wakati wa kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki,wengine katika picha(kulia) ni mtaalamu wa mifumo ya kompyuta Michael Kanakakis,waliokaa (kutoka kulia) ni Dimitrios Lintis na Zakaria Kanyi.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Mrisho Millao(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto) wakati wa kuchezesha droo ya nne ya Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni moja kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akiwasiliana na mmoja wa washindi wakati wa kuchezesha droo ya nne ya Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni moja kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.kushoto kwake ni msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Millao.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Januari 18, 2015
WATEJA watano wa Vodacom Tanzania wamejishindia milioni 1 kila mmoja wao katika droo ya tatu na ya nne ya promosheni ya Jaymillions iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Washindi hao ni Janeth Peter Nganyange,mjasiriamali na mkazi wa Njombe,Stanley Bagashe mkazi wa Shinyanga na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Ibizamanta,Evarista Minja mkazi wa Mwanza na mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Ramadhan Hamis Maulid mkazi wa Dodoma ambaye ni mkulima na Walter Minja ambaye ni Dalali.
“Nimefurahi sana kwa kushinda milioni 1 kupitia promosheni ya Jaymillions kwa kuwa kwa kiasi kikubwa fedha hizi  zitanisaidia kupanua biashara yangu na kununulia watoto wangu mahitaji mbalimbali”.Anasema Janeth Peter Nganyange (40) mkazi wa Njombe mmoja wa washindi.

Nganyange amesema ushindi huu umeleta faraja kubwa kwake na familia yake ikizingatiwa kwamba miezi mitatu iliyopita alifiwa na mme wake na kumuachia familia yenye watoto wawili ambao anahangaika nao kuwalea. “Mungu ni mkubwa na ushindi huu umeleta faraja kubwa kwangu na nashukuru Vodacom kwa kubadilisha maisha yangu kwa maana kwa muda mrefu nilikuwa nahangaika kutafuta mkopo wa kuendeleza biashara yangu bila mafanikio”, anasema.
Mteja mwingine aliyejishindia milioni ni Walter Minja,mkazi wa Mbezi beach  jijini Dar es Salaam ambaye ni mwajiriwa ambaye pia amesema kuwa amefurahia  kuibuka mshindi hasa katika kipindi hiki cha mwezi wa kwanza ambao unakuwa ni mgumu kwa watu wengi.
“Nafurahi kujishindia milioni moja ya Jaymillions na itanisaidia sana kuvuka katika mwezi huu mgumu wa Januari ambao unakuwa na  mambo mengi.Nashukuru Vodacom kuandaa promosheni hii na nawahimiza watanzania wenzangu kushiriki kwa kucheki namba zao za simu kama zimeshinda “.Amesema Minja.

Stanley Bagashe mkazi wa Shinyanga na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Ibizamanta amesema amefurahi kupata ushindi na fedha hizo zitamsaidia kutimiza ndoto yake ya muda mrefu wa kufungua duka la M-Pesa “Fedha hizi zimekuja wakati muafaka naamini ndoto yangu ya kufungua duka la M-pesa imetimia”.Alisema.
Mshindi mwingine Evarista Amedeus Minja mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine amesema amefurahia kujishindia  milioni 1/- za Promosheni ya Jaymillions na zitamsaidia kukamilisha masomo yake. “Fedha hizi zimepatikana katika wakati mwafaka na zitanisaidia kulipia gharama za hosteli na kumalizia utafiti wangu kwa kuwa sipati mkopo kutoka Bodi ya Mikopo”.Alisema kwa furaha.

Naye Ramadhan Maulid alisema amefurahia ushindi huu na fedha hizo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo “Nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii na nawasihi watanzania wenzangu tuendelee kushiriki“. alisema.

Mbali na washindi hao wa fedha taslim wateja wengi wamejishindia muda wa maongezi.

Kwa upande wake ,Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia amewapongeza washindi na kuwahimiza wateja wote wa Vodacom kuangalia namba zao kila siku kama zimeshinda kwa kutuma ujumbe mfupi  wenye neno JAY kwenda namba 15544  ili wasipoteze nafasi zao za kushinda.

“Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions itakayofanyika kwa siku 100 mfululizo inawahusisha wateja wote wa Vodacom ,kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”, alisema.

Vodacom imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-

No comments:

Post a Comment