Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi akieleza lengo la ziara ya kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji mkoani Mtwara kwa Mkuu wa mkoa huo Mwantumu Mahiza (kushoto).Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Asaa Hamadi.
Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi, akieleza jambo wakati alipowasili kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Lindi tayari kukagua miradi ya maji.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Nassor Himid na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Mathei Makwinya.
Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi, akizungumza na viongozi wa mradi wa maji wa Rondo-Mnara na kata ya Mnara.
Mhandisi wa Maji mkoa wa Lindi Valentine Ndyano (aliyevaa shati la kitenge) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge kuhusu mtambo wa kusukuma maji.
Msafara wa ziara ukirejea mjini baada ya kukagua mtambo.
Mhandisi wa Maji mkoa wa Lindi Valentine Ndyano akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge kuhusu mtambo wa kusambaza maji kwenye vituo vya maji.
Meneja wa Mradi wa Maji wa 7 Towns Upraging Program Kanali Mstaafu Rajendra Kumar akieleza jambo kuhusu mradi huo.
Wajumbe wakikagua maendeleo ya mradi huo unaotarajiwa kukamilika Machi mwaka huu.
Meneja wa
Mradi wa Maji wa 7 Towns Upraging Program Kanali Mstaafu Rajendra Kumar,
akiashiri jambo wakati alipowatembeza wajumbe kwenye mradi huo.
Na Hussein
Makame, MAELEZO, Lindi
WANANCHI
waliopo kwenye maeneo ya miradi ya maji mkoani Lindi na nchini kwa ujumla wametakiwa
kuacha kuzembea kwenye vikao vya kujadili maendeleo ya miradi hiyo kwani
kufanya hivyo kutachangia kufa kwa miradi hiyo.
Hayo yamesemwa
na Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
mkoani Pwani, Lindi na Mtwara Amina Makilagi (Mb) wakati alipotembelea mradi wa
maji wa Rondo-Mnara uliopo katika kijiji cha Mnara Kata za Mnara na Chiponda
wilaya ya Lindi mkoani Lindi.
Alisema
miradi mingi ya maendeleo imekufa kutokana na wananchi kuzembea kwenye vikao
vya kujadili uendeshaji wa miradi ya maji, hivyo kuwafanya viongozi wasio
waaminifu kutumia vibaya fedha za miradi hiyo.
“Mnachotakiwa
msizembee kwenye vikao vya kujadili miradi ya maji kwani mkifanya hivyo miradi
itakufa kutokana na viongozi kutumia vibaya fedha za miradi hiyo kujinufaisha
wenyewe” alisema Makilagi.
Alisema
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia utaratibu wa kuingiza fedha za miradi
ya maendeleo ya maji kwenye akaunti kwani kufanya hivyo kutaepusha viongozi
wabadhirifu kuihujumu miradi hiyo.
Akisoma
taarifa ya mradi huo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo ya bunge, Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Lindi Olliver Vavunge alisema mradi wa Rondo-Mnara
ulisanifiwa kuhudumia wakazi 18,000 kwenye vijiji sita.
Alisema
mradi huo uliojengwa na serikali mwaka 1973 una uwezo wa kuzalisha mita za maji
zenye ujazo wa 450 kwa siku lakini kutokana na changamoto ya uchakavu wa
mitambo na gharama kubwa za uendheshaji, uzalishaji umepungua hadi mita za ujazo 328 kwa siku.
“Vituo vitatu vya kusukua maji vilijengwa
kutoka kwenye chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Chikote.Ambapo kwenye
kila kituo ilifungwa mitambo miwili ya kusukuma maji iliyotumia injini ya diseli.”
Alisema Vavunge.
Alisema
mradi wa Rondo-Mnara ni miongoni mwa miradi minne ya maji safi na salama ambayo
hadi sasa imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi ikiwemo miradi ya Kiwawa,
Likwaya na Namkongo.
“Miradi hiyo
inatoa huduma ya maji kwa wakazi 5,000 huku halmashauri ikiendelea kutekeleza
miradi ya Maji ya Namangale, Hingawali, Littipu, Nyangamara na Nahukahuka”
alisema.
Kwa upande
wa mradi wa Ng’apa unaojulikana kwa jina la 7 Towns Upgrading Program,
unaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani na Jumuiya ya Ulaya, una lengo la
kuboresha huduma ya maji katika mji wa Lindi.
Mradi huo
unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka huu na kufikisha huduma ya maji safi
na salama kwa wakazi 194,143 wa manispaa ya Lindi na unajenga mtambo wa
kusafisha majitaka yanayozalishwa katika mji wa Lindi.
Awali
akiwasilisha taarifa ya huduma ya maji mkoa wa Lindi kwa wajumbe wa kamati hiyo
ya Bunge mkoani Lindi, Afisa Tawala wa Mkoa wa Lindi Abdallah Chikota alisema
hadi Novemba mwaka 2014 wakazi wa mijini wanaopata maji safi ni asilimia 55.4
ya wakazi wote 162, 049.
Alisema kwa
upande wa wakazi wa vijijini wanaopata huduma ya maji safi na salama
wanakadiiriwa kufikia 297,796 kati ya wakazi 702, 603 wa vijijini.
Naye Mkuu wa
mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza alisema pamoja na Serikali kutoa fedha kwa ajili
ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa mkoa huo, lakini huduma
hiyo haipatikani kama inavyotakiwa kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme
ambao kwa siku unaweza kukatika kati ya mara 22 hadi 25.
Hata hivyo,
alisema amewasilisha taarifa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na
wanatarajia kukutana na uongozi wa juu wa shirika hilo hivi karibuni ili
kujadili changamoto hiyo ambayo inategemewa kwa kiasi kikubwa katika
upatikanaji wa maji mkoani humo.
Ziara ya
wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji inaendelea kukagua miradi
ya maji katika mkoa wa Mtwara ambapo inatarajia kukagua miradi ya
Nanyamba-Namkuku na Tandahimba-Matogolo.
No comments:
Post a Comment