TANGAZO


Sunday, January 11, 2015

Simba yaipiga Polisi Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Aman mjini Zanzibar

*Kucheza Fainali na Mtibwa Sugar Jumanne

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuaza mchezo wa Nusu Fainali ya pili kati ya Simba na Polisi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan, Simba imeshinda bao 1-0, Itacheza fainali na timu ya Mtibwa baada ya kuitoa timu ya JKU kwa penenti 4-3. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews Blog)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasalimia wachezaji wa timu ya Polisi kabla kuaza kwa mchezo wao na timu ya Simba. Mchezo uliofanyika uwanja wa amaan
Kikosi cha timu ya Simba kilichoilaza timu ya JKU katika mchezo wa Nusu Fainal, uliofanyika uwanja wa Amaan.
Wachezaji wa Timu ya Polisi wakiomba dua kabla ya mchezo wao kuaza wa Nusu Fainal uliofanyika uwanja wa Amaan, Timu ya Simba imeshinda bao 1-0.
Kikosi cha timu ya Polisi kilichopambana na timu ya Simba katika mchezo wa Nusu Fainali uliofanyika uwanja wa Amaan. 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akijumuika na wananchi na Viongozi wa ZFA, kuangalia mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, kati ya Simba na Polisi uliofanyika uwanja wa Amaan. 
Mshambuliaji wa timu ya Simba Jonas Mkunde, akijiandaa kumpita beki wa timu ya Polisi Adam Juma, wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan.
Mshambuliaji wa timu ya Simba Elias Maguri akijiandaa kumiliki mpira, huku beki wa timu ya Polisi akimzuia asilete madhara galini kwao. 
Wachezaji wa Simba Elias Maguri akikimbilia mpira huku beki wa timu ya Polisi Mohammed Haji akiwa karibu kuokoa mpira huo.
Mchezaji wa timu ya Polisi akiwania mpira huku beki wa timu ya Simba akimkimbilia.

Mshambuliaji wa timu ya Simba Ramadhani Singano, akishangilia bao lake la kwanza na la ushindi kwa timu yake dhidi ya timu ya Polisi wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan.

Mshambuliaji wa timu ya Simba Dan Sserenkuma, akimpita beki wa timu ya Polisi Juma Ali, katika mchezo wao wa kuwania kucheza Fainali ya Kombe la Mapinduzi. 
Mshambuliaji wa timu ya Simba Elias Maguri na beki wa timu ya Polisi Mohammed Haji wakiwania mpira huo.

No comments:

Post a Comment