TANGAZO


Sunday, January 11, 2015

CRDB Lumumba, Yaadhimisha Siku ya Huduma kwa Wateja Kwa Kuwakumbuka Wenye Ulemavu

Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi, mkikabidhi zawadi ya vifaa vya shule kwa watoto wenye ulemavu, wanaolelewa katika kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi, mkikabidhi zawadi ya vifaa vya shule kwa mtoto mwenye Ulemavu wa ngozi, Aisha Omary, wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Benki ya CRDB Tawi la Lumumba.
Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi, mkikabidhi zawadi ya vifaa vya shule kwa mtoto mwenye Ulemavu wa ngozi , Mery Muhingila, wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Benki ya CRDB Tawi la Lumumba.
Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi, mkikabidhi zawadi ya vifaa vya shule kwa mtoto mwenye Ulemavu wa Viungo,Veronica Mbogela, katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Benki ya CRDB. 
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, wakijumuika pamoja na pamoja na watoto wenye ulemavu, wanaolelewa katika kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, wakishiriki kuwahudumia watoto wenye ulemavu, wanaolelewa katika kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB, Tawi la Lumumba, katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu, wanaolelewa katika kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam.    

Na Mwandishi wetu
11/01/2015  
CRDB Bank Tawi la Lumumba,  Yaukaribishwa mwaka , kwa Kutembelea Kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam.

Huku wakiongozwa na Mkurugenzi wa  CRDB Tawi la Lumumba, John Almasi, wafanyakazi hao, walijumuika na watoto hao, kwa kuwapa zawadi mbalimbali, na kushiriki kutoa huduma mbalimbali shuleni hapo.

Akizungumzia kuanza kwa mwaka, Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Lumumba, John Almasi, amesema wameamua kuanza mwaka kwa  kuwakumbuka watu wenye uhitaji, kwa vile CRDB ni Benki ya  Jamii, na watu wenye uhitaji pia ni sehemu ya jamii, hivyo wameonelea ni bora waadhimishe, kwa kutembelea na kuwasawadia watoto wenye ulemavu wa kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini.
Wakiishukuru benki hiyo, mwakilishi wa watoto hao, Mary Mwingira, aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwakumbuka na kuwajali, na akatoa wito kwa taasisi nyingine, ziige mfano wa CRDB kwa kuwakumbuka.
Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Joseph Masasi pia aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuwakumbuka watu wenye ulemavu wa ngozi, na kukumbushia, watu hao wana changamoto za mahitaji ya ziada, yakiwemo mafuta mazito ya kuzuia miale ya jua.

Benki ya CRDB, imewakabidhi zawadi mbalimbali, watoto hao, vikiwemo vifaa vya shule na vyakula mbalimbali.

No comments:

Post a Comment