Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, kati ya timu yao na Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo na Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba akijaribu kumpiga chenga Aggrey Morris wa Azam FC, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Emmanuel Okwi akijaribu kumpiga chenga Shomari Kapombe wa Azam FC, wakati wa mchezo kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Emmanuel Okwi akiwania mpira na Shomari Kapombe wa Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mchezaji Wawa wa Azam FC, akiwa amedondoka chini huku akiwania mpira na Said Ndemla (kulia) wa Simba, wakati wa mchezo huo. Kushoto ni Elias Maguri wa timu hiyo.
Agrey Morris wa Azam FC, akijaribu kuutoa mpira miguuni mwa Dan Sserunkuma na Emmanuel Okwi wa Simba.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiwa amebebwa akitolewa nje baada ya kuumizwa, wakati timu yake ilipokuwa ikipambana na Azam Fc, Uwanja wa Taifa, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1.
Emmanuel Okwi wa Simba, akiwa amebebwa akitolewa nje baada ya kuumizwa, wakati wa mchezo huo.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akitolewa nje kwa machela, baada ya kuumizwa, wakati timu yake ilipokuwa ikipambana na Azam Fc, Uwanja wa Taifa, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1.
Emmanuel Okwi akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumizwa, wakati timu yake ilipokuwa ikipambana na Azam Fc, Uwanja wa Taifa, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Khamisi Mussa)
No comments:
Post a Comment