*Wafanyakazi watoa misaada kwa wazee wa Nunge, Kigamboni
*Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kawawa watembelea Ofisi za Posta Kuu (Mpya), Dar es Salaam
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kawawa, Luhanga Mabibo, wakipatiwa maelezo kuhusu uchambuzi wa barua na vifurushi na Ester Zakayo wa Kitengo cha Box, wakati walipotembelea Posta Kuu, Dar es Salaam leo, ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Posta Afrika, inayoadhimishwa nchini kesho. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kawawa, Luhanga Mabibo, wakipatiwa maelezo kuhusu uchambuzi wa barua na vifurushi vinavyopotea na Mkuu wa Ketengo na Ofisa Mwandamizi, George Lugan wa Kitengo cha Box, wakati walipotembelea Posta Kuu, Dar es Salaam leo, ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Posta Afrika, inayoadhimishwa nchini kesho.
Ofisa Ustawi wa Jamii, Ojuku Mgedzi, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Posta, walipotemmbelea Makao ya wazee, Nunge, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao leo.
Ofisa Mwandamizi Mkuu wa Mahusiano wa Shirika la Posta Tanzania, Wilfred Miigo akizungumza wakati wa hafla hiyo, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Posta Afrika, yanayoadhimishwa kesho.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania, Elia Madulesi akizungumza wakati wa hafla hiyo, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Posta Afrika, yanayoadhimishwa kesho.
Ofisa Uhusiano Mwandmizi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Joseph Ngowi akiwa na Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hudson Mwakitalu, wakati wa hafla hiyo, kwenye Kambi ya wazee hao leo.
Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hudson Mwakitalu, akizungumza jambo wakati wa wakati wa hafla hiyo, kwenye Kambi ya wazee hao leo. Ikiwa ni katika sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Posta, duniani kesho.
Ofisa Ustawi wa Jamii, Ojuku Mgedzi, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Posta, walipotemmbelea Makao ya wazee, Nunge, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao leo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakiwa katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta wakiwa katika Makazi ya wazee wasiojiweza ya Nunge, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo, wakati walipofika kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao.
Kaimu Meneja wa Shirika la Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Hudson Mwakitalu, akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo kwa wazee hao leo.
Baadhi ya wazee wasiojiweza wa Makao ya Nunge, Kigamboni wakiwa katika hafla hiyo leo.
Kaimu Meneja wa Shirika la Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Hudson Mwakitalu, akimkabidhi Ofisa Ustawi wa Jamii, Ojuku Mgedzi, fedha kwa ajili ya kuwalipia ada za shule watoto wa wazee hao.
Kaimu Meneja wa Shirika la Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Hudson Mwakitalu, akimkabidhi Ofisa Ustawi wa Jamii, Ojuku Mgedzi, moja ya katuni za sabuni kwa ajili ya wazee hao.
Kaimu Meneja wa Shirika la Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Hudson Mwakitalu, akimkabidhi Ofisa Ustawi wa Jamii, Ojuku Mgedzi, moja ya katuni za sabuni kwa ajili ya wazee hao.
1.0 UTANGULIZI
Tumekutana hapa leo ili kuwapa
taarifa kuwa kesho Shirika la Posta Tanzania (TPC) litaungana na wadau wote wa
posta kwenye Bara la Afrika ili kuadhimisha kwa pamoja siku ya posta katika
bara hili kwa mwaka huu kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni:-
“USIMAMIZI
WA SEKTA YA POSTA: DHIMA YAKE NI KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA HII”
Siku hii ni kumbukumbu ya kutia saini
mjini Arusha, makubaliano yaliyoanzisha Umoja na Posta Barani Afrika PAPU tarehe
18 Januari ,mwaka 1980 na hivyo kuwezesha umoja huu kuwa Shirika tanzu la Umoja
wa Afrika (AU). Kwa hiyo, nchi yetu ya Tanzania ndiye mwenyeji wa Makao Makuu
ya Umoja huu yaliyoko Jijini Arusha. Kesho Umoja huo utatimiza miaka 35.
Umoja huu una nchi wanachama 43 kwa
sasa. Kwa ufupi katika PAPU, chombo cha
juu cha maamuzi ni mkutano mkuu wa Mawaziri wenye dhamana ya mawasiliano ambao
hufanyika kila baada ya miaka mine (4). Chombo kingine ni Baraza la Utawala
ambao husimamia maamuzi ya mkutano mkuu wa Mawaziri na chombo hiki husaidiwa na
kamati za ufundi zipatazo sita ambazo zinajumuisha
§ Maendeleo ya TEHAMA na uboreshaji wa
huduma za posta na fedha.
§ Kamati ya kuboresha huduma za barua
na usalama wa mfumo wa Posta.
§ Kamati inayoshughulikia na kutetea
maslahi ya Afrika kwenye mambo muhimu ulimwenguni.
§ Kamati nyingine ni ya Maendeleo ya
Posta na mahusiano ya kimataifa na kujenga uwezo wa Rasilimali watu.
§ Na kamati ya masuala ya mikakati ya
kibiashara.
Shughuli za kila siku za PAPU husimamiwa na Katibu Mkuu (Secretary
General) pamoja na watendaji wengine wa Secretariati hiyo iliyoko Arusha.
2.0
DHIMA YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
Kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia sekta ya
mawasiliano kwa njia ya Posta hapa nchini,
Shirika la Posta Tanzania ndilo lenye dhima ya kutoa huduma kwa umma
(DPPO) kwa kuhakikisha huduma za msingi za mawasiliano haya ya Posta zinawafikia Wananchi wote.
Dhima hii imezingatiwa pia katika
Sheria iliyoanzisha Shirika hili ambayo pamoja na mambo mengine inaelekeza:-
·
Kuweka
mipango ya kuhakikisha huduma za msingi za Posta zinapatika nchini kote ili
kukidhi mahitaji ya msingi ya mawasiliano kwa jamii nzima ya watanzania
(Universal Service Obligation).
·
Kutoa
huduma za uwakala na huduma nyingine zinazohitajika kwa jamii kupitia mtandao
wa Posta kwa lengo la kuliimarisha Shirika hili kiuchumi na pia kuchochea
maendeleo ya Sekta na Taasisi nyingine.
·
Kuchangia
juhudi za Serikali za usambazaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) ili teknolojia hiyo ichangie maendeleo ya Taifa na irahisishe
uendeshaji wa maisha na shughuli za kila siku za wananchi.
3.0
UTEKELEZAJI WA DHIMA HII NA KAULI
MBIU YA MWAKA HUU
Kwa kuzingatia dhima hii ya Shirika
la Posta Tanzania na kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya siku ya Posta
Barani Afrika Shirika linachukua hatua zifuatazo:-
MIPANGO YA MAENDELEO
Maadhimisho haya yanafanyika wakati
Shirika la Posta Tanzania limetimiza miaka 21 tangu kuanzishwa kwake tarehe 1
januari, 1994. Tangu wakati huo yamekuwako mafanikio ya kuridhisha sana ingawa
pia zimekuwako changamoto kadhaa.
Mwaka jana Shirika la Posta Tanzania
lilianza utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka 10. Hatua hii inazingatia
juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kupitia utekelezaji wa sera na mipango
mbalimbali ikiwa ni pampja na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 (Vision 2025),
Mpango wa “Matokeo makubwa kwa sasa” (Big Result Now) na sera ya Taifa ya Posta
(National Postal Policy 2013).
Mpango huo kabambe wa Shirika ni
mwendelezo wa mikakati mipya itakayoleta mabadiliko katika uendeshaji na utoaji
wa huduma za Posta nchini ili kukabiliana na changamoto zinazotolewa na
mabadiliko ya teknolojia, kukidhi mahitaji ya soko na kukabiliana na ushindani.
La muhimu zaidi ni kupanua wigo na kuboresha huduma tukizingatia kauli mbiu ya
siku ya Posta Barani Afrika ya mwaka huu.
4.0 UBORESHAJI
WA HUDUMA
Hatua mojawapo tunazozichukua ni
kutekeleza mradi wa kuunganisha (on-line) mtandao wa Ofisi za Posta 140 kwa
kutumia mfumo wa teknolojia ya kisasa. Kwa hivi sasa ofisi 97 tayari
zimeshaunganishwa na mwaka huu Ofisi zote kamili zaidi ya 140 Posta
zitaunganishwa katika mfumo huu.
Aidha, tunao upimaji na usimamizi wa
ubora wa ubora unaofanyika kwa utaratibu ufuatao:-
ü Ndani ya mji (intra-town)
tunahakikisha kuwa mtu anayetuma barua, vifurushi, nyaraka , vipeto au vitu
vyovyote ndani ya mji aliopo anafikishiwa kwa mtumiwa siku hiyo hiyo.
ü Kati mji na mji (inter-town). Katika miji
mingi hapa Tanzania tunahakikisha mtumiaji anafikishiwa vitu vyote kwa mtumiwa
siku inayofuata.
ü Vile vile tunao utaratibu wa
kuzingatia ubora katika ngazi za Wilaya na Vijiji.
ü Hatua nyingine tuliyoichukua, ili
kuzingatia ubora ni kuwa kwa hivi sasa kwa
papo hapo tumeboresha zaidi mfumo wa kupata kwa urahisi na bila usumbufu
taarifa za barua na vifurushi kupitia tovuti yetu www.posta.co.tz.
Chini ya usimamizi wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Shirika linashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) katika kubuni na kuweka mikakati ya utekelezaji wa mfumo wa
anuani za makazi na postkodi (physical Addressing System & Post Code
System). Wadau wengine muhimu ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Serikali za Mtaa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
5.0 HUDUMA ZA USAMBAZAJI NA LOGISTIKI
Sambamba na utekelezaji wa mfumo wa
Anuani za Makazi na Simbo za Posta, tunazingatia kuwa mahitaji ya huduma za
usambazaji, usafirishaji na logistiki yanaongezeka kwa kasi sana duaniani kote.
Kwa mfano wananchi wengi wangependa wafikishiwe mahitaji yao pale pale walipo
au wanapopataka wao na kwa muda mfupi. Baadhi ya wadadisi wanahoji kuwa huduma
za kiwango hiki ni vigumu kutolewa hapa nchini pengine kutokana na makazi
holela na kutakuwako na utashi wa watendaji. Shirika la posta tunawahakikishia
kuwa tunao uzoefu, utashi, dhamira na uwezo wa kutoa huduma hizi kwa kiwango
cha kuridhisha. Tangu mwaka 1985 tumekuwa tukitoa huduma katika mfumo huu
kupitia huduma ya EMS na kwa hivi sasa zimesambaa katika mikoa yote.
6.0 UPANUZI WA WIGO WA HUDUMA
Shirika limechukua hatua kubwa ikiwa
ni pamoja na kuanzisha huduma mpya ili kupanua wigo wa huduma zote. Hatua hii
ni pamoja na:-
·
Kampuni ya Tanzu ya Posta Bureau De
Change: Shirika
limeanzisha Kampuni Tanzu ya kuuza na kununua fedha za kigeni kwa lengo la
kuwafikishia wananchi huduma za kifedha. Duka la kwanza limefunguliwa Dar es
Salaa. Mpango wa muda mrefu ni kufungua maduka mengine katika posta kuu za
Arusha, Tunduma, Zanzibar na sehemu
nyingine ambako makampuni binafsi hayatoi huduma hii.
·
Biashara ya City Urgent Mail/CUM:
Shirika limeanzisha huduma ya kusambaza barua, nyaraka na vipeto kwa
haraka ndani ya miji (intracity mail) na tayari miji mingi ya mikoa pamoja na
Zanzibar imeanza kutoa huduma hiyo. Nia yetu ni kuanzisha huduma hii katika
miji yote ya mikoa na baadhi ya Wilaya, ifikapo mwisho wa wa mwaka huu.
·
Huduma za Fedha na Uwakala:
Shirika limeendelea kuimarisha huduma zake za kifedha kama vile kutuma
na kulipa fedha zinazotumwa kupitia mtandao wa kielektroniki chini ya huduma ya
posta cash. Kwa sasa vituo 97 vimeunganishwa kwa nchi nzima na mwaka huu ofisi
140 zitaunganishwa katika mfumo wa Post-Global unaowezesha pesa kutumwa na
kulipwa papo kwa hapo.
·
Huduma za POSTGIRO: Ndani ya huduma hizi wateja hupata
huduma za kupokea na kulipa fedha katika utaratibu wa uwakala kama ifuatavyo:-
ü Malipo ya Gawio:
ü Kuuza na kununua hisa:
ü Malipo ya Pensheni kwa naba ya Mifuko
ya Jamii:
ü kifedha kutokana na mikopo midogo na
mikubwa inayotolewa kwa masharti nafuu.
7.0 HITIMISHO
Pamoja na matokeo mengine muhimu,
matokeo halisi ya dhamira ya Shirika ni kuhakikisha kuwa watanzania wanafaidika
na matunda ya huduma bora na za kisasa za mawasiliano ya posta ambayo ni pamoja
na kuwarahisishia upatikanaji wa huduma
za kibiashara na fedha (financial inclusion), Elimu, Afya bora, kuwaongezea
kasi katika matumizi ya sayansi na teknolojia, kuwapunguzia umaskini na kwa
ujumla kuwarahisishia uendeshaji wa maisha yao ya kila siku.
Tumejipanga vizuri na tuna imani
kubwa ya kutekeleza dhamira yetu hii.
Imetolewa:
KITENGO CHA MAWASILIANO
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
DAR ES SALAAM
17 JANUARI, 2015
No comments:
Post a Comment