Shirika la la ndege la Uturuki ambalo ndilo liliokuwa peke yake likiendesha shughuli zake nchini Libya, limesimamisha safari zake zote kuingia nchini humo kutokana na hali mbaya ya usalama.
Shirika hilo lilisimamisha safari zake kwenda mji wa Misrata siku ya Jumatatu na kusema kuwa halitaendelea na huduma zake kwenye miji mingine ikiwemo mji mkuu Tripoli, Benghazi na Sebha.
Libya kwa sasa inakabiliwa na ghasia zinazohusiana na kung'ang'ania madaraka kati ya serikali inayotambuliwa kimataifa na waasi wa kiislamu.
Siku ya Jumatatu serikali ya Libya iliomba muungano wa kiarabu kuisadia na silaha ili kuweza kukabiliana na wanamgambo wanaozorotesha hali ya usalama nchini humo.
Makampuni mengi nchini humo yamekuwa yakiendesha shughuli zao katika uwanja wa Mitiga mjini Tripoli. Lakini uwanja huo uliposhambuliwa mwishoni mwa wiki, makamapuni hayo yakalazimika kufunga virago.
Libya imekumbwa na utovu wa usalama tangu kung'olewa mamlakani kwa aliyekuwa mtawala wa nchi hio, Muammar Gaddafi mwaka 2011, na vurugu zimekuwa zikiongezeka katika miezi ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment