Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nzega, Bw. Abrahaman Mndeme akipokea barua pamoja na hundi zenye jumla ya kiasi cha shilingi millioni 21 kutoka kwa Afisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni.
Ofisa
Vijana wa Halmashauri ya Nzega, Bi. Frida Lwani (watatu kulia)
akifafanua jambo kuhusu maendeleo ya vikundi vya vijana vya hapo kwa Maafisa kutoka Wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipowatembelea katika Ofisi ya Halmashauri ya Nzega hivi karibuni.
Na Anitha
Jonas – Maelezo,Nzega
SERIKALI imewataka vijana kuitumia vyema mikopo wanayopata katika kuteketeza miradi
mbalimbali ya kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa
Ufutiliaji na Tathimini toka
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi.Verdiana Mushi wakati
alipotembelea Ofisi ya Halmashauri ya Nzega na kwa ajili ya kukabidhi hundi ya
kiasi cha shilingi milioni 21 itakayosaidia kukopesha vikundi vya vijana
walioko chini ya Vijana Saccoss Nzega.
“Serikali
inaendelea kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi kwa
kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ambayo
itawaongezea kipato na kuwaondolea umasikini kwani vijana ndiyo nguvu kazi ya
nchi” Alisema Bi.Mushi.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nzega Bw. Abrahaman Mndeme ameishukuru serikali
kwa kuwapatia mkopo huo vijana wa Nzega kwani kwa kupitia mkopo huo vijana
watafaidika sana na pia watachangia kukua kwa pato la Halmashauri na kupunguza
vijana wanaoka vijiweni na kushauriana mambo yasiyo na maendeleo katika jamii.
“Uongozi
wa Halmashauri kwa kushirikiana na Saccoss ya Vijana Nzega utasimamia gawio la
fedha hizo kwa vikundi husika na kuhakikisha miradi iliyoandikwa na vikundi
hivyo inatekelezwa, pamoja na kufuatilia urejeshwaji mikopo hiyo kwa wakati ili
vikundi vingine viendelee kunufaika na mikopo hiyo inayotolewa na
serikali”,alisema Bw.Mndeme.
Akitoa
hamasa kwa vijana Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo Bw.Eliakim Mtawa aliwaasa Vijana kuunda vikundi na kujiunga katika
Saccoss za Vijana zilizopo katika halmashauri zao ili waweze kuomba mkopo utakao wasaidia kufanya shughuli mbalimbali
za kiuchumi badala ya kukaa vijiweni.
“Serikali
imedhamiria kwa dhati kuwakomboa vijana kiuchumi kwa kutambua changamoto ya
ajira iliyopo katika taifa letu kwa sasa
na dunia nzima kwa ujumla”,alisema Bw.Mtawa.
Pamoja
na hayo naye Mwenyekiti wa Vijana Saccoss Nzega Bw.Emmanuel Mambo, ameishukuru
serikali kwa niaba ya vijana wa Nzega kupitia Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni
na Michezo na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuwapatia fedha hizo walizoomba kwa
ajili ya kufanya miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji na kilimo itakayoongeza kipato
chao.
No comments:
Post a Comment