TANGAZO


Monday, January 12, 2015

Ridhiwani aanza kutimiza ahadi, Awashukuru wananchi kwa kumchaagua Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akimkabidhi Diwani wa Kata ya Miono. Senguli Mbele moja kati ya matairi manne aliyonunua kwa ajili ya gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Miono, wakati wa mkutano wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua miezi sita iliyopita. Mkutano huo ulifanyika jana katika Kata ya Miono, Chalinze, wilayani Bagamoyo, Pwani.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.(Picha zote na Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog)
Mmasai mwenye jamii ya kifugaji Andokela Okunge akiuliza swali kwa Mbunge Ridhiwani kuhsu Jamii sivyowaendea haki wafugaji ambapo alidai kuwa mkulima anaweza kuuzi shamba halafu baadaye anageuka na kusema amedhulumia jambo ambalo si kweli.
Mwajabu Hemedambaye ambaye nyumba yake ilibomoka, akilalamik mbele ya Mbunge Ridhiwani kuwa alipotoa taarifa y kusaidiwa ujenzi wa yumba hiyo kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, alijibiwa kwa dhiahaka kuwa amkubalie aklale naye kwanza ndipo amsaidie.
Mzee Msoud Mhina akilalamika mbele ya Munge Ridhiwani kuwa Serikali ya CCM imewasahau wazee kwa kutowahudumia hali ambayo inawafanya waishi maisha magumu.
 Mkazi wa Miono, Sahaban Mpwimbwi akimuomba Mbunge Ridhiwani awasaidie katika Kata ya Miono kukarabati Rambo la maji ambalo limehribika. Rambo hilo lilijengwa Enzi Rais Jakaya Kikwete akiwa mbunge wa jibo la Chalinze.
Ridhiwani akijadiliana jambo Diwani wa Kata ya Miono Senguli Mbele huku kwaya Kijiji ikitumbuiza na kutoa maneno ya matatizo yaliyopo katika Kituo cha Afya ch Miono ikiwemo kukosekana kwa chumba cha upasuaji ka waja wazito.
Ridhiwani akisalimiana na wazee wa Miono
Wafugaji wakijadiliana jambo a Mbunge Ridhiwani mjini Miono.
Ridhiwani akisalimiana na watoto alipowasili katika Kijii cha Kweynkonje, Kata ya Miono.
Sehemu ya wananchi walihudhuria mkutano katika Kijiji cha Kweynkonje.
Mzee Khatib Yusufu akielezea jinsi walivyofurahi kutembelewa na Mbunge wao Ridhiwani atik Kijiji cha Kweynkonje
Ridhiwni akisalimiana na Bibi Khadija Ibrahim lipowasili katika Kijiji cha Kweynkonje.
Mkazi wa wa Kijiji cha Masimbani Kassim Mwakibindu 968) ambaye amesoma darasa moja  na Rais Jakaya Kikwete Kidato cha nane katika Shule ya Sekondari ya Lugoba, Chalinze wilayani Bagamoyo, Pwani, akimuomba Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kuendeleza juhudi za Rais Kikwete kwa kuwajali kwa maendeleo wakazi wa kijiji hicho kilichopo kata ya Miono.

M
Saumu Bakari akimuomba Ridhiwani kusaidia kununua jokofu la kuhifadhia chanjo na dawa katika Zahanati ya Kijiji hicho.
Ridhiwani akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Masimbani ambapo aliwashukuru na kuahidi kutekeleza ahadi mbalimbali alizoziahidi wakati wa kampeni.

No comments:

Post a Comment