TANGAZO


Wednesday, January 14, 2015

Rais Shein awakabidhi Simba Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Mtibwa Sugar, Uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup Bi Shery Khamis akiongozana na Rais Shein kwenda kukabidhi zawadi kwa washindi wa Kombe hilo. mchezo uliofanyika uwanja wa amaan. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Said Mbarouk, kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup Bi Shery Khamis, Rais wa ZFA Ravia Idarous na Rais wa TFF Ndg.Jamal Maliz wakiwa katika jukwaa la kukabidhi zawadi kwa washindi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waamuzi waliochezesha mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Mtibwa Sugar, uliofanyika katika uwanja wa Amaan, timu ya Simba imeshinda kwa penenti 4--3. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwavisha nishani washindi wa Pili wa Kombe la Mapinduzi timu ya Mtibwa. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi fedha Nahodha wa timu ya Mtibwa Sugar, zawadi ya mshindi wa pili fedha taslim. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimvisha Nishani ya Dhahabu kipa wa timu ya Simba  Ivo Mapunda. baada ya timu yao kuibuka Bingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Akisalimiana na Kocha wa Simba. 
Rais Shein akimkabidhi Nahodha wa Simba, Is-haka Hassan Fedha baada ya kuwa bingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Rais Shein, akilinyanyua juu Kombe hilo.
Rais Shein akimkabidhi Nahodha wa Simba, Is-haka Hassan Kombe la Ubingwa huo.
Rais Shein akipiga picha ya pamoja na wachezaji wa Simba, mara baada ya kuwakabidhi Kombe na Fedha baada ya kushinda Ubingwa huo.
Kocha wa Simba akiwa  amelishikilia Kombe la Mapinduzi.
Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Simba, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Muhamed Shein usiku wa kuamkia leo baada ya kuifunga Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penalti 4-3, Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar usiku wa kuamkia leo.

No comments:

Post a Comment