TANGAZO


Tuesday, January 13, 2015

Rais Dk. Mgeni rasmi Tarab ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar Hoteli ya Bwawani

Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Pili Seif Iddi (kulia) akiwa na Waziri wa Kilimo na Maliasili Dkt. Sira Ubwa Mamboya wakiwa katika Taarab rasmi ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyocharazwa na kikundi cha Taifa cha Culture Muzical Club katika ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, (Picha zote na Ikulu) 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akiwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, Said Ali Mbarouk (kulia), Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis wakiwa   katika Taarab rasmi iliyocharazwa na kikundi cha Taifa cha Culture Muzical Club katika ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Unguja jana katika kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya wananchi na mashabiki wa Taarab waliohudhuria katika hafla ya Taarab hiyo ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyocharazwa na kikundi cha Taifa cha Culture Muzical Club katika ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Unguja jana. 
Waimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Muzical Club, Asha Ali  na Khamis Nyange, wakiimba wimbo wa miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar uliotungwa na Profesa Gogo mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.
Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Muzical Club Saada Mohammed akiimba wimbo uanosema  "kweli nnae" wakati wa Taarab rasmi ya kusherehekea miaka  51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.
Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Muzical Club Mtumwa Mbarouk akiimba wimbo wa "Mpewa hapokonyeki" wakati wa Taarab rasmi ya kusherehekea miaka  51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mbele ya mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment