TANGAZO


Tuesday, January 6, 2015

Miss Tanzania 2013 awashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono

Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea mafanikio yake na pia kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono kipindi chote cha mashindano ya urembo ya duni yaliyofanyika hivi karibuni. Kushoto ni mshindi wa Pili wa Miss Tanzania 2014, Jihan Dimachk. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akifafanua jambo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuelezea mafanikio yake na pia kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono kipindi chote cha mashindano ya urembo ya duni yaliyofanyika hivi karibuni. Kushoto ni mshindi wa Pili wa Miss Tanzania 2014, Jihan Dimachk.
Waandishi wa habari, wakimsikiliza Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa (hayupo pichani), alipoluwa akielezea kuhusu mafanikio aliyoyapata na pia kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono kipindi chote cha mashindano ya urembo ya duni yaliyofanyika hivi karibuni. 
Waandishi wa habari, wakimsikiliza Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa (hayupo pichani), alipoluwa akielezea kuhusu mafanikio aliyoyapata na pia kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono kipindi chote cha mashindano ya urembo ya duni yaliyofanyika hivi karibuni. 
Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio yake na pia kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono kipindi chote cha mashindano ya urembo ya duni yaliyofanyika hivi karibuni. Kushoto ni mshindi wa Pili wa Miss Tanzania 2014, Jihan Dimachk.
Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akizungumza jambo mshindi wa Pili wa Miss Tanzania 2014, Jihan Dimachk mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam.

Na Celina Mathew
ALIYEKUWA Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa amewashukuru watanzania kwa sapoti waliompa kipindi chote alichokuwa kwenye mashindano ambapo walimwezesha kupata nafasi ya pili kwa upande wa warembo wanaopendwa duniani.

Aidha, Tanzania imekua nchi ya 2 kati ya nchi 121 zilizoshiriki katika shindano hilo la kumtafuta mrembo anayependwa duniani.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Watimanywa alisema alipaswa kushika nafasi yakwanza lakini kutokana changamoto mbalimbali zilizojitokeza aliweza kushika nafasi ya pili.

Kama ningepata nafasi ya kwanza, ningeweza kuingia katika 10 bora katika mashindano ya dunia (Miss World), hivyo mshindi aliyeshika nafasi ya kwanza alifanikiwa kuingia kwenye mashindano ya kutafuta mrembo wa dunia.

Hata hivyo alisema mashindano yalikuwa na changamoto lakini  kutokana na sapoti alizopata toka kwa watanzania zilimwezesha kupata nafasi hiyo na kwamba warembo wengine walishinda kutokana na sapoti nzuri waliopewa kutoka kwenye nchi zao.

"Mashindano ni maandalizi toka nyumbani, hivyo jinsi ulivyoandaliwa ndio unavyoweza kupata ushindi, kwenye maandalizi kulikuwa kuna watu waliozaidi yangu hivyo watanzania tunatakiwa tulichukulie suala hilo kama somo ,"alisema.

Aidha alisema kuwa alipata sapoti kubwa toka kwa Bodi ya Utalii Tanzania kwa kuonesha video yake hivyo kumuwezesha kuitangaza nchi, pamoja na kutangaza madini ya Tanzanite.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine aliyokutana nayo ni pamoja na kupewa vifaa ambavyo havikutosha kwa mahitaji ya siku alizokuwa kwenye mashindano hayo.
"Inabidi tuige mifano ya nchi ntingine zinavyofanya ili kuwawezesha warembo wao kushinda kwa kuwapa sapoti kubwa,"alisema.
Wakati huo huo Watimanya alisema kuwa anatarajiwa kurudi shuleni , lakini kabla ya kwenda anatarajiwa kubuni baadhi ya vitu ambavyo vitamsaidia katika kuendelea kutangaza nchi.

No comments:

Post a Comment