TANGAZO


Sunday, January 11, 2015

Mbunge Ridhiwani Kikwete akabidhi Ambulance Kituo cha Afya Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama. (Picha zote na Richard Mwaikenda, Kamanda wa Matukio Blog)
Muumini wa Dini ya Kikiristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.
Dk. Mastidia Rutaihwa, akimkabidhi ufunguo wa gari hilo, Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk. Victor baada ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.
 Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance.
 Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa.
Mbunge Ridhiwani Kikwete na Dk. Rutaihwa wakiangalia ndani ya ambulance hiyo.
Wakiwa na furaha baada ya kuangalia samani zilizomo ndani ya ambulance hiyo.
 Ridhiwani  pamoja na viongozi wa dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo. Kutoka kulia ni Alhaji  Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula.
Ridhiwani 9katikati) na Mbuunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Mastidia Rutaihwa akitoa shukurani kwa Ridhiwani kwa msaada wa Ambulance na kuahidi kuitunza.
Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo.
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya ambulance katika viwanja vya miembe saba mjini Chalinze jana.
Mbunge wa Jimbo la Mtera, Dodoma, Lusinde ambaye alikuwa safarini akitokea Dodoma kwenda Dar kwenye vikao vya Kamati za Bunge, aliamua kushiriki kwenye mkutano huo ambapo alimsifia Mbunge Ridhiwani kwa kipindi kifupi alichoaguliwa kuwa mbunge miezi sita iliyopita kutekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ambulance hiyo, ujenzi wa visima katika vijiji mbalimbali na ujenzi wa barabara pamoja na zahanati.
Lusinde akikumbatiana kwa furaha na Ridhiwani baada ya mkutano huo kumalizika.

No comments:

Post a Comment