TANGAZO


Monday, January 12, 2015

Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein (kulia), akizungumza jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, wakati wa Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar leo. (Picha zote na Freddy Maro/ Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili Uwanja wa Amaan tayari kwa maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mjini Unguja leo.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa wakati wa maadhimisho hayo.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye maadhimisho hayo ya Mapinduzi ya Zanzibar.




Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kikosi cha FFU  wakitoa
heshima ya gwaride la mwendo wa haraka kwa Mgeni rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan leo.


Askari wa Jeshi la Wanamaji Zanzibar Kikosi cha KMKM  wakitoa heshima kwa gwaride la mwendo wa haraka kwa Mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein  katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan leo.
Askari wa Kikosi cha Mafunzo Serikali ya Zanzibar (SMZ), wakipita mbeke ya Mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa mwendo
wa pole katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan leo.




Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum
za SMZ wakipita mbele ya jukwaa kwa maandamano wakati wa sherehe za Kuadhimisha miaka 521 ya mapinduzi ya Zanzinar akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar
zilizofanyika leo, Uwanja wa Amaan Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment