Hafsa Mtasiwa, Kamanda wa vijana wa CCM, Wilaya ya Iringa Vijijini, mkoani Iringa, akikabidhi fomu fomu.
HAFSA
MTASIWA Kamanda wa Vijana wa CCM, Wilaya ya Iringa vijijini, Mkoani akiapa kuwa Mkuu wa Wilaya Pangani.HAFSA MTASIWA Kamanda wa Vijana wa CCM, Wilaya ya Iringa Vijijini, mkoani Iringa, akisimikwa kuwa Kamanda wa vijana.
Na Fredy Mgunda, Iringa
HAFSA
MTASIWA Kamanda wa vijana wa CCM Wilaya ya Iringa vijijini, mkoani
hapa, ambaye pia ni Mkuu wa Wiliya ya Pangani, mkoani Tanga, amesema kuwa vijana
wanawajibu kwa kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa manufaa ya jamii
katika maendelo.
Wito
umetolewa kwa Vijana mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla
kujiandikisha katika tafutari la kudumu ili waweze kupata
vitambulisho vya kudumu pamoja na kujitokeza kupiga kula katika
katiba iliyopendekezwa.
Amewataka
wanawake kuondoa woga na kuuvaa ujasiri na kuwa na ushirikiano katika
kugombea uongozi katika sekta mbalimbali kwani nafasi hizo
hazibagui jinsia.
Aidha, ametoa wito kwa wanchi na viongozi wa Serikali kudumisha amani na pia
kuliombea taifa kupata viongozi walio bora katika uchaguzi mkuu ambao
unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
“Eti
asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na
kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi
na nini nyumbani”, alisema Hafsa Mtasiwa.
Mtasiwa ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au
kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi
wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na
ndio sababu inayopelekea hata watu wazima
kurudi shuleni.
kurudi shuleni.
“Vijana
mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma
kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto
maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”, alisema Hafsa Mtasiwa.
Lakini
HAFSA MTASIWA Kamanda wa vijana wa CCM Wilaya ya Iringa vijijini, mkoani Iringa amewataka akinamama kujitokeza kwa wingi kugombea
nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi
wa kumi mwaka huu.
MTASIWA
ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na
ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo
yasiyokuwepo.
Ameendelea
kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na
badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka
katika chama chochote.
Aidha
ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea
haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali
na hayo MTASIWA
amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa
katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa
kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea
kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo
katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa
haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la
wapiga kura pamoja na kupiga kura.
No comments:
Post a Comment