Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Juma Duni Haji, akisoma tamko la chama hicho, mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kulaani Jeshi la Polisi kwa kile alichodai kutumiwa kuhujumu Demokrasia nchini. Kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa, Bonifasia Mapunda. (Picha na Kassim Mbarouk)
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema kitaendelea na masimamo wake wa kuandamana kila mwaka kwa ajili ya kuwaenzei na kuwakumbuka wenzao na kulitaka jeshi la Polisi nchini kukaa mkao kwa mapambano na wananchi kwani maandamano hayo yatakuwa ni ya kila mwaka.
Aidha kimesema kuwa licha ya vurugu zilizotokea mwaka huu, maadhimisho hayo, ambayo hufanyika kila mwaka kwa mwaka 2016, yatakuwa makubwa zaidi kulingana na jeshi hilo litakavyo kabiliana nayo.
Kauli hiyo, imekuja siku chache baada ya Mwenykiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na wananachama wengine 32 wa chama hicho, kushikiliwa na jeshi la polisi kwa kudaiwa kufanya maandamano kinyume na taratibu.
Baada ya kushikiliwa na jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Januari 27, mwaka huu Prof. Lipumba alihojiwa na kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la kushawishi wafuasi wake kufanya kosa la jinai, ambapo kesi yake, iliahirishwa na kuwa itatajwa tena Febduar 26 mwaka huu.
Mbali na Mwenyekiti huyo, kufikishwa mahakamani na kusomewa shtaka hilo, pia leo wanachama wengine, wakiwemo viongozi wa juu wa chama hicho Taifa, wamefikishwa mahakani kusomewa mastaka hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Juma Duni Haji, amesema kuwa chama hicho, kimesikitishwa na kinalaani vikali kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi na kudai kuwa ni kitendo cha udhalilishaji.
"Sisi tunalishangaa jeshi la polisi kwani kama kuwakamata wangewakamata wakati maandamano hayo yalikuwa anatarajia kuanza maeneo ya Temeke Hospitali kwani ndio kulikuwa na malumbano ambayo Mwenyekiti aliyatuliza na kuwatawanya wananchi kusitisha maandamano na mkutano na ikawa hivyo.
"Cha kushangaza wameenda kuwakama Mtoni Mtongani sehemu ambayo haikuwa na vurugu ya aina yeyote wakati Prof. Lipumba akielekea Mbagala Zakhem ambapo mkutano ulitarajiwa kufanyika kwaajili ya kutoa taarifa ya kusitishwa kwa mkutano huo," alisema Haji.
Haji alilitaka jeshi hilo kutekeleza majukumu yake kwa kutumia weledi na kubainisha kuwa wasipofanya hivyo jeshi litaiingiza nchi katika ghasia na vurugu ambazo athari zake hazitakuwa kwa upande mmoja pekee.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha CUF, Joran Bashange, alibainisha kuwa Lipumba haumwi Presha bali hali ya ugonjwa iliyojitokeza wakati akihojiwa na jeshi hilo imesababishwa na hali ya vurugu iliyojitokeza wakati akikamatwa hadi kuhojiwa na jeshi la polisi.
Alisema kuwa hadi sasa hali yake inaendelea vizuri na kwamba amepewa mapumziko kwa siku tatu bila kujihusisha na chochote ili afya yake iweze kutengemaa.
Alisema sehemu kubwa ya uongozi huo ilikumbwa na hali hiyo na leo (jana) wamepelekwa mahakani na kubainisha kuwa hadi sasa wamebaki viongozi wawili tu ambao hawakukamatwa.
"Sisi tunasubiri na hawa waliobaki kwani mwenyekiti ameshitakiwa kwa kosa la jinai ambalo halifahamiki na hawa wengine wamefikishwa mahakamani leo (jana) kwa kosa ambalo halifahamiki kwani hakukuwa na maandamano," aliongeza Mkurugenzi huyo.
Naye Kada wa CUF Cormani Marwa alisema kuwa kulikuwa hakuna sababu ya msingi kwa Jeshi la Polisi kutumia nguvu katika kudhibiti maandamano ya Chama cha wananchi CUF, kwani walipaswa kusikilizana na kufikia makubaliano kwa njia ya maridhiano.
Siku chache zilizopita Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibraham Lipumba alikutana
na kipigo kutoka kwa Jeshi la Polisi baada ya kukiuka amri ya jeshi hilo la kupinga kufanyika kwa maandamano ya kuwakumbuka watanzania waliopoteza maisha yao miaka 14 katika vuruguza kisiasa zilizotokea visiwani Zanzibar mwaka 2001.

No comments:
Post a Comment