Cameroon na Guinea zilitoka sare ya 1-1 na kuzifanya timu zote katika kundi la D katika mechi za mataifa ya Afrika kuwa sawa kwa pointi.
Mechi zote nne zimetoka sare ya 1-1,ikimaanisha kuwa maswala mengi yataangaziwa iwapo timu hizo zitapata matokeo ya sare jumatano ijayo.
Cameroon ilionekana kuwa juu ya kundi hilo wakati Benjamin Moukandjo alipofunga moja kwa moja kutoka kona aliyopiga.
Lakini Ibrahima Traore alisawazisha kutoka yadi 20 na kuzua wasiwasi mwingi katika mechi za mwisho zitakazochezwa jumatano ili kupata kiongozi wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment