Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akisoma majumuisho ya michango na ahadi zilizotolewa na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya kuchangia maendeleo ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jana usiku jijini Dar es salaam. Kiasi cha shilingi milioni mia tano arobaini, laki nane na elfu ishrini na tisa (540,829,000/=) zikiwa ni ahadi na fedha taslimu zilikusanywa.
Mmoja wa wadau wa maendeleo wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakitoa ahadi na michango mbalimbali kusaidia maendeleo ya chuo hicho jana usiku wakati wa chakula cha hisani cha miaka 50 ya CBE kilichoandaliwa na uongozi wa chuo hicho kusaidia ukusanyaji wa fedha za ujenzi wa miundombinu,vyumba vya mihadhara na madarasa vya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho. (Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE wakitoa mkono wa shukrani kwa wadau mbalimbali waliotoa michango yao wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha CBE jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Janeth Mbene, akitoa mchango wake mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE, wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha hicho usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Wananchi, wasomi na wafanyakazi wa Chuo cha CBE, wakitoa michango yao, mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd na viongozi wa Chuo cha CBE, wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha hicho usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam, wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akizungumza wakati wa Harambe hiyo, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Janeth Mbene na kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Profesa Mathew Luhanga.
Na Othman Khamis Ame, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar22/1/2015.
JUMLA ya sh. mil. 540.8 zimechangwa katika hafla ya harambe ya kuchangia Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, huku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akiongoza harambe hiyo.
Pia, mbali na fedha keshi zilizokusanywa vile vile kulikuwa na ahadi ya fedha iliyotolewa na baadhi ya watu waliosoma chuo hicho na wale wanaofanya shughuli zao kwenye chuo hicho.
nyengine kutolewa ahadi na wakereketwa mbali mbali
Fedha hizo zimechangwa kwa ajili ya upanuzi wa chuo, ambapo majengo mengine yanategemewa kujengwa kwa ajili ya kukipanua chuo hicho.
Kati ya fedha hizo, Shilingi Milioni 400,000,000/- pekee zimechangwa na wahadhiri, Wafanyakazi, Walimu na wanafunzi wa chuo hicho na shilingi Milioni 104,479,000/- zilizotolewa ahadi na washirika mbali mbali wa maendeleo ya Elimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliongoza harambe maalum ya kuchangisha fedha hizo kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa na Uongozi wa Chuo hicho hapo Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa chakula hicho, walionekana kuhamasika vyema kuchangia mfuko huo baada kuelewa changamoto
zinazokikabili chuo cha Elimu ya Biashara hasa uchakavu na ufinyu wa majengo ya chuo hicho sambamba na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Wananchi na wadau mbali mbali nchini kwa utayari wao wa kuchangia
sekta ya elimu hapa Nchini.
Balozi Seif alisema Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikikabiliana na changamoto zinazotokana na
sekta ya elimu.
Alisema upanuzi wa ubora wa elimu nchini umekuwa ukifanywa ili kuwapa fursa wasomi kuvitumia vizuri vipaji vyao na hii inatokana na kipaumbele kilichowekwa ndani
ya mpango wa maendeleo ambao sekta ya elimu imepewa nafasi pana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi pamoja na Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa malengo uliojiwekea kwenye mpango huo wa kukusanya
shilingi Bilioni moja.
“ Kwa nini tusiendelee kuchangia maendeleo ya elimu sisi wenyewe badala ya nguvu nyingi kuzitumia kwenye harusi na mambo mengine ya hanasa “. Alisema Balozi Seif.
Alielezea faraja yake kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu uliopo Tanzania uliopelekea kuongezeka kwa idadi ya vyuo vya elimu ya juu ambapo kwa sasa vimefikia 60.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara Profesa Matthew Luhanga alisema ipo haja ya kuhamasishwa wananchi wajikite zaidi katika kuhakikisha kwamba watoto wao wanapata elimu ya juu.
Profesa Luhanga alisema asilimia 44% ya vijana kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wahudumiwe ipasavyo katika kupatiwa elimu itakayowawezesha kujidumu kimaisha.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara alieleza kwamba uharibifu mkubwa unaofanywa nchini unatokana na vitendo vya Vijana waliokosa elimu.
No comments:
Post a Comment