Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wanawake kutoka
Kinondoni akifunga penati wakati wa fainali za Copa Coca Cola 2014 katika
mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mapema wikiendi
hii, Kinondoni ilinyakua ubingwa kwa kuifunga
Ilala mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili
mbili.
Mashabiki wakifuatilia fainali za Copa Coca Cola 2014, Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.
Dkt. Fenella Mukangara (MB) (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia mara baada ya
kukabidhi zawadi ya mchezaji bora wa
kike katika mashindano ya Copa Coca Cola kwa Golikipa wa timu ya Kinondoni
Zubeda Mohamed (15). Wakwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Coca Cola Bw.
Godfrey Njowoka, Rais wa TFF Jamal Malinzi na nyuma ya waziri anayecheka ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo.
Wachezaji wa timu ya Dodoma wakifurahi baada ya kukabidhiwa zawadi zao za ubingwa wa michuano ya Copa Coca Cola baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa mwaka 2014 kwa mashindano hayo kwa kuichapa Kinondoni jumla ya magoli 4 -0, wakati kwa upande wa wanawake Kinondoni ilinyakua ubingwa kuifunga Ilala kwa mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)
No comments:
Post a Comment