TANGAZO


Friday, December 5, 2014

Wataka Sokwe apewe haki za kibinadamu

Sokwe Tommy anaaminika kuwa na umri wa miaka 40
Sokwe hawana haki sawa na binadamu na wala sio lazima wanyama hao kuachiwa huru na wale wanaowafuga. Hii ni kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama nchini Marekani.
Uamuzi huu ulitolewa katika kesi kumhusu Sokwe kwa jina Tommy ambaye wanahakatari wa kutetea wanyama walitaka aachiliwe huru na mmiliki wake na pia atunzwe kama binadamu.
Jaji katika mahakama ya rufaa mjini New York aliyeisikiliza kesi hio, amesema Sokwe wanaokuwa wamefugwa hawawezi kutunzwa sawa na binadamu kwani hawawezi kuwajibishwa kama anavyoweza binadamu.
Shirika moja la kutetea haki za wanyama lilikuwa limedai kuwa Sokwe walio na usawa fulani na binadamu wanapaswa kuwa na haki sawa na na binadamu ikiwemo kupewa uhuru.
Shirika hilo limesema litakata rufaa katika kesi hiyo.
Katika uamuzi wake , jaji aliandika: '' Sokwe hawawezi kuwa na haki sawa na binadamu kwani hawawezi kuwajibishwa wala kupewa majukumu.''
Mahakama hio iliongeza kuwa hakuna sheria inayoshurutisha kwamba wanyama hao wapewe haki sawa na binadamu.
Mnamo mwezi Okotoba, shirika hilo la kutetea haki za wanyama, lilikuwa limetetea kwamba, Sokwe wanapaswa kutambuliwa kama binadamu katika sheria, na kisha kupewa haki sawa na uhuru kama binadamu.
Shirika hilo limesema litakata rufaa dhidi ya hukumu hio katika mahakama ya juu zaidi nchini humo.

No comments:

Post a Comment