TANGAZO


Friday, December 5, 2014

Kauli ya Uhuru Kenyatta kwenye Twitter

Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto.
Baadhi wanahisi kuwa waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi watakosa haki ingawa baadhi wanahisi kwua Uhuru Kenyatta hakupaswa hata kufikishwa ICC tangu hapo.
Lakini swali ni jee Rais Kenyatta alipokea vipi habari hiyo?
Rais Uhuru Kenyatta
Haya ndio aliyokuwa nayo ya kusema kwenye akaunto yake ya Twitter:
  • ''Nimepokea habari kwamba kiongozi wa mashitaka ICC ametupilia mbali kesi dhidi yangu ........''
  • ''Daima nimekuwa nikisema kuwa kesi za Kenya ICC ziliharakishwa sana kupelkewa katika mahakama ya ICC bila kufanyiwa uchunguzi wa kina.
  • "moyo wangu hauna shauku hata kjidogo. ''
  • "mara kwa mara nimekuwa nikiwasisitizia wakenya na dunia nzima kuwa sina hatua. ''
  • "uamuzi huu ni afueni kubwa sana kwangu kwani ulipaswa kutolewa miaka sita iliyopita. Umechelewa sana ''
  • ''Nimefurahishwa sana na habari hizi ambazo nimekuwa nikizisubiri tangu jina langu kuhusishwa na kesi iliyowasilishwa Hague dhidi yangu.''
  • ''Kadhalika Naibu wangu William Ruto ni kiungo muhimu sana kwa serikali yangu na ninathamini umuhimu wake''

No comments:

Post a Comment