TANGAZO


Wednesday, December 3, 2014

Wanafunzi 9 wahitimu mafunzo ya uuguzi ukunga kwa udhamini wa Barclays Bank kupitia kampeni ya “Stand Up For African Mothers” inayoendeshwa na Amref Health Africa - Tanzania

Dk. Pius Chaya, Mkuu wa Kitengo cha kujenga uwezo Amref Health Africa Tanzania, akimwakilisha Mkurugenzi, Dk. Festus Ilako, akiongea katika mahafali ya Chuo cha Muheza School of Nursing mkoani Tanga hivi karibuni.
Miongoni mwa wanafunzi 121, waliohitimu uuguzi  ngazi ya Cheti, miongoni mwao wakiwemo tisa (9), waliofadhiliwa na Barclays kupitia  Stand up For African Mothers Campaign inayoendeshwa na Amref Health, wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao.
Mkuu wa Chuo cha Muheza School of Nursing mkoani Tanga, akiwa pamoja na viongozi na wakufunzi wengine katika picha ya pamoja, wakati wa mahafali hayo hivi karibuni.
Mkuu wa Chuo hicho, akiwa pamoja na viongozi na baadhi ya wakufunzi wengine, katika  picha ya pamoja.
Mkuu wa Chuo hicho, Baba Askofu pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja, wakati wa mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu pamoja na wanafunzi wanaoendea na masomo yao ya uuguzi ngazi ya cheti wakifurahia, wakati wa mahafali hayo.
 Wahitimu wakila kiapo cha kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu.
Wanafunzi waliohitimu kwa kufafadhiliwa na Barclays Bank kupitia kampeni  ya Amref Health Africa ya Stand Up For African Mothers, wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu
RASILIMALI watu ni changamoto kubwa inayoikabili sekta ya afya nchini Tanzania. Upungufu huu unaathiri mfumo wa utoaji huduma bora na kwa wakati kwa wahitaji. Upungufu wa wahudumu wa afya  wenye ujuzi unaathiri ngazi zote za huduma na hasa vijijini. 
Kutokana  na wauguzi wakunga kuwa kiini katika utoaji  huduma za afya   vijijini na mijini kwa ujumla,  kuna umuhimu wa  wakunga hawa kupata elimu ya ujuzi  wa kutosha ili waweze kuwafikia wahitaji zaidi ya asilimia  sabini ( 70%)  ya  jumla ya wananchi wanaoishi vijijini.
Katika kupambana na changamoto ya upungufu wa wahudumu wa afya hasa katika kulenga  kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, Amref Health Africa imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha taasisi, mashirika na watu binafsi kuchangia mafunzo ya wakunga watalaam   ili waweze kutoa huduma salama, sahihi na kwa wakati ili kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika wakati wa kujifungua.
Jumla ya Wanafunzi 121 wamehitimu mafunzo ya uuguzi ukunga ngazi ya cheti katika chuo cha Muheza School of Nursing mkoani Tanga.  
Miongoni mwa wanafunzi hao 9 walikuwa wakisoma kwa udhamini wa Barclays bank kupitia kampeni ya “Stand up for African Mothers” inayoendeshwa na Shirika la afya la Amref Health Africa Tanzania.
Barclays Bank ni mshiriki mkubwa katika kampeni hii  na anatoa udhamini wa kusomesha wanafunzi  katika ngazi ya cheti na hivi leo  tumeshuhudia  wanafunzi 9 wamehitimu tayari kwa kwenda kutoa huduma katika jamii zinazowazunguka. Wahitimu hawa wanakwenda kufanya kazi maeneo ya vijijini Kama moja ya lengo na nia ya kampeni ya stand up for African mothers ambayo inalenga kupunguza vifo vya mama na mtoto hasa maeneo ya kijijini na yaliyo magumu kufikika.
Juhudi za Amref Health Africa na Barclays bank  ni endelevu  na wito unatolewa  kwa mashirika, makampuni ya umma na yale ya binafsi, pamoja na watu binafsi  kuunga mkono jitihada hizi kwa kudhamini mafunzo ya wakunga (mafunzo ya mkunga  kwa miaka miwili  yanagharimu dola 3000). Unaweza kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia

·         Bank  account at Bank M, Kisutu Branch , Akaunti Namba  0250027331
·         Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, Akaunti Namba 0111030004548
·         Mpesa Namba 0762 22 33 48
·         Tigo pesa Namba 0716 032 441
·         Airtel money Namba 0685 506306.
Stand Up For African mothers ni kampeni ya kimataifa inayolenga kuelimisha na kutoa taarifa juu ya umuhimu na mchango wa wakunga wenye ujuzi katika kupunguza viofo vya mama na watoto wakati wa kujifungua.  Kampeni hii inayoendeshwa na Amref Health Africa inalenga kusomesha wakunga 15,000 katika nchi kumi na tatu za Africa wakati Tanzania ikitarajia kusomesha wakunga 3800.

Kuhusu Amref Health Africa.
Amref Health Africa ni Taasisi kongwe ya afya  ya  kimataifa  isiyo ya kiserikali , inayotoa mafunzo na  huduma za afya  kwa zaidi ya nchi 30  barani  Africa.   Shirika hili lilianzishwa mwaka 1957 kama “AMREF flying Doctors” kwa ajili ya kutoa huduma muhimu za kiafya katika jamii iliyokuwa katika maeneo magumu kufikika.
  
Kwa sasa, Amref Health Africa inatoa huduma nyingi za afya katika jamii na hasa kwa kuzingatia  wanajamii wahitaji ambao wengi wanaishi katika maeneo magumu kufikika barani Afrika. 

Amref Health Africa imejikita  katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya, mafunzo and ujengaji uwezo , mikakati ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na mtoto, UKIMWI, kifua kikuu, malaria, maji safi na usafi wa mazingira,  huduma za madaktari bingwa na maabara.

Amref Health Africa inabaki kuwa  Taasisi ya mfano na  kuaminika  kimataifa kwa  kuwezesha utolewaji wa huduma bora za afya  na endelevu kwa  miaka 57 toka kuanzishwa kwake mwaka 1957.
Kwa mawasiliano zaidi, Wasiliana na Eliminatha Paschal,
Kitengo cha Habari na Mawasiliano-Amref Health Africa Tanzania,
 Mobile: 0767 555958

No comments:

Post a Comment