TANGAZO


Wednesday, December 3, 2014

Tuzo ya mashindano ya utunzi wa vitabu vya watoto kwa lugha ya Kiingereza

Katibu Mtendaji wa Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania (MVWT), Pilli Dumea, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuanza kwa shindano la tuzo la uandishi wa vitabu vya lugha ya Kiingereza kwa watoto, ijulikanayo kama 'Burt Award African Literature' (BAAL). Kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo, Ramadhani Ali.
Katibu Mtendaji wa Mradi wa Vitabu vya Watoto Tanzania (MVWT), Pilli Dumea, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuanza kwa shindano la tuzo la uandishi wa vitabu vya lugha ya Kiingereza kwa watoto, ijulikanayo kama 'Burt Award African Literature' (BAAL). Kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo, Ramadhani Ali. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Na Mwandishi wetu
WATANZANIA wametakiwa kujifunza na kusoma kwa bidii vitabu vya riwaya vinavyoandikwa  kwa lugha ya Kingereza ili kupata uelewa wa mambo mbalimbali yanayotokea nchini.


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mradi wa Vitabu vya Kingereza, Pili Dumea wakati akizindua mradi wa saba wa mashindano ya uandishi wa riwaya za Kingereza.
Alisema Mashindano hayo yatajumuisha nchi ya Kenya, Ethiopia, Canada na Tanzania ambapo lengo la mashindano hayo ni kutaka kufahamu vipaji vya uandishi nchini.

"Kumekuwa na changamoto nyingi za uhaba wa vitabu vya kingereza hapa nchini kwani vingi vinatoka kwa wenzetu jambo ambalo hatulihitaji hata kidogo, hivyo mashindano haya yatasaidia kuongeza idadi ya vitabu nchini na wasomaji,"alisema.


Dumea aliongeza mashindano haya pia yatasaidia kujenga ari na upenzi katika kusoma na kujua kingereza na hata kukuza ukuaji wa viwanda vya kutengeneza vitabu na hatimaye kukuza uchumi wa nchi.
Pia alitaja jinsi ya kushiriki katika mashindano hayo ni lazima mtu awe mtanzania na pia lazima aandike kitu cha kumfanya msomaji afikirie sana na pia lazima atumie misamiati rahisi.


"Washindi watakaopatikana  katika mashindano hayo wa kwanza atafanikiwa kupata milioni 14,wapili atapata milioni 11 na watatu atapata milioni nane,"alisema.

No comments:

Post a Comment