TANGAZO


Saturday, December 6, 2014

Wanafunzi 1,044 wahitimu Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam leo

Wahitimu wa digrii ya  elimu jamii katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa  digrii hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu "Kuelekea modeli ya mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog)
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu (Doctor of Phylosophy Degree), Deusdedit Kibassa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo. Mada ya utafiti aliyoifanya inahusu: "Umuhimu wa kutumia maeneo ya kijani kupunguza athari zitokanazo na kuongezeka kwa hali ya joto katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam."
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Dawah Mushi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Mada  ya utafiti aliyoifanya Mushi  inahusu: "Uhamishwaji wa makazi ya watu wengi waliobomolewa makazi yao katika mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam."
 Daniel Mbisso akitunukiwa Digrii ya Uzamifu.
Joel Msami akitunukiwa Digrii ya Uzamifu.
 Eliwaha Msangi akitunukiwa Digrii ya Uzamifu.
 Margareth Ntiyakunze akitunukiwa Digrii ya Uzamifu.
 Sara Phoya akitunukiwa digriii ya uzamifu.
 Baadhi ya wahitimu wakipiga picha wakati wa mahafali hayo.
 Bendi ya JKT ikiongoza maandamano ya viongozi na wahadhili wa chuo hicho kuingia ukumbini.
Wahadhiri na viongozi wakiingia kwa maandamano kwenye ukumbi.
Baadhi ya wahitimu wakisubiri kutunukiwa digrii zao.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi, Tabitha Siwale akihutubia katika mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrissa Mcharo akihutubia wakati wa mahafali hayo.
 Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), wakiweka kofia kichwani ikiwa ni ishara ya kutunukiwa digrii ya uzamili ya sayansi ya usimamizi na uchumi ujenzi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Ni furaha iliyoje baada ya kutunukiwa digrii zao.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Waziri Mkuu wa zamani, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha ARU, Cleopa Msuya akitoka baada ya mahafali hayo kumalizika leo.
Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika.
Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika.

No comments:

Post a Comment