Askari Polisi wakiwa wamejiweka tayari na gari lao, kudhibiti fujo zozote zitakazotokea kwenye kituo cha kupigia kura cha Mtambani, Vingunguti, Dar es Salaam leo, wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulioaghirishwa kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza wiki iliyopita. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Askari Polisi akiwataka wananchi waliokwisha kupiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Mtambani, Vingunguti, Dar es Salaam kuondoka kwenye eneo hilo, ili kuondoa msongamano, wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulioaghirishwa kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza wiki iliyopita.
Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura cha Mtambani, Vingunguti, Dar es Salaam, akiwalekeza waandikishaji kunza kuhesabu kura mara baada ya muda wa kupiga kura kuisha, wakati wa uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ulioaghirishwa kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza wiki iliyopita.
Mwananchi mkazi wa Mtaa wa Alimaua, Kijitonyama, akipigakura kumchagua Mwenyekiti na Wajumbe wa Serikali ya mtaa huo, wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulioaghirishwa kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza wiki iliyopita.
Wakazi wa Mtaa wa Alimaua, Kijitonyama, wakiangalia majina yao kwa ajili ya kwenda kupigakura za kuwachagua Mwenyekiti na Wajumbe wa mtaa huo leo.
Askari Polisi wakimuhoji mkazi wa Mtaa wa Alimaua, Kijitonyama, aliyekuwa akizunguka huku na kule, wakati upigaji kura ukiendelea, kuwachagua Mwenyekiti na Wajumbe wa mtaa huo leo.
Askari Polisi wakiwazuia wananchi waliokwisha kupiga kura wasisogelee kwenye eneo la upigaji kura katika Kituo cha upigaji kura cha Mtaa wa Alimaua, Kijitonyama, Dar es Salaam leo.
Wakazi wa Mwenge Kijijini, wakiingia kwenye chumba cha kupigia kura kwenda kuwachagua viongozi wa mtaa huo, huku askari Polisi wakiwaangalia kwa makini.
Mkazi wa Mwenge Kijijini, akipewa karatasi za kupigia kura kwenye chumba cha kupigia kura kwenda kuwachagua viongozi wa mtaa huo, Dar es Salaam leo.
Kijana mkazi wa Buguruni Mnyamani, akiwaeleza jambo askari kazu, waliokuwa wakilinda usalama kwenye kituo cha kupigia kura cha mtaa huo.
Mwananchi mkazi wa Buguruni Mnyamani, akijaza karatasi za kupigia kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa mtaa huo, wakati wa uchaguzi wa kuwachagua Mwenyekiti na wajumbe wa Serikali ya Mtaa. Wiki iliyopita uchaguzi huo, uliaghirishwa kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza.
Wananchi wakazi wa Buguruni Mnyamani, wakiwa wamejikusanya nje ya Kituo cha Kupigia kura kwa ajili ya kuwatambua wananchi wasiokuwa wakazi wa maeneo hayo, wasijitumbukize kwenye zoezi hilo kwa ajili ya kuwasaidia wagombea.
Wakazi wa Vingunguti, Mtaa wa Faru, jijini Dar es Salaam, wakimalizia zoezi la kupiga kura, huku muda wa mwisho ukiwa unakaribia kumalizika.
Baadhi ya wakazi wa Vingunguti, Mtaa wa Faru, jijini Dar es Salaam, wakisubiri kuhesabiwa kwa kura baada ya zoezi la upigaji kura kuwachagua viongozi wa mtaa huo, kukamilika leo jioni.
Baadhi ya akinamama wakazi wa Vingunguti, Mtaa wa Faru, jijini Dar es Salaam, wakisubiri kuhesabiwa kwa kura baada ya zoezi la upigaji kura kuwachagua viongozi wa mtaa huo, kukamilika jioni ya leo.
No comments:
Post a Comment