Wananchi na wanachama wa Chama cha wananchi CUF kisiwani Pemba, wakimsikiliza Mwenyekiti wa chama hicho taifa Pro: Ibrahim Harouna Lipumba, alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika skuli ya Jadida Wete Pemba.
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Taifa Profesa Ibrahim Harouna Lipumba, akikabidhi gari aina ya ‘Noah’ kwa uongozi wa jimbo la Mtambwe, iliotolewa na mwakilishi wa jimbo hilo Salim Abdalla Hamad, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika skuli ya Jadida Wete Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazuri, akitoa salamu zake kwa wanachama wa chama cha wananchi CUF kisiwani Pemba, kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliohutubiwa na Mwenyekiti wa chama hicho taifa Pro: Ibrahim Harouna Lipumba uliofanyika skuli ya Jadida Wete Pemba.
Wananchi na wanachama wa Chama cha Wananchi CUF kisiwani Pemba, wakinua mikono yao juu, wakiashiria kutoiunga mkono katiba iliopendekezwa ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanachama hao walikuwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika skuli ya Jadida Wete Pemba.
Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa salamu kwa wanachama wa chama cha wananchi CUF kisiwani Pemba, kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliohutubiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Profesa Ibrahim Harouna Lipumba, uliofanyika skuli ya Jadida Wete Pemba.
Makamu Mwenyekiti wa CUF Mhe: Juma Duni Haji akizungumza na wanachama wa chama hicho kisiwani Pemba, kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika skuli ya Jadida Wete Pemba, na kuhutubiwa na mwenyekiti wa chama hicho Taifa Profesa Ibrahim Harouna Lipumba.
Mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Ibrahim Haroun Lipumba akiwahutubia wafuasi wa chama hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika skuli ya Jadida Wete mkoa wa kaskazini Pemba.
No comments:
Post a Comment