TANGAZO


Sunday, December 14, 2014

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Dar es Salaam

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Mkwajuni, Kigamboni, Salum Chimbyoka, akitoa maelekezo kwa wananchi wakati wa upigaji kura wa serikali ya mtaa huo, Dar es Salaam leo. 
Msimamizi wa uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Mwembe Poa, Tungi, Kigamboni, Stelia Ungele (wapili kushoto), akimwelekeza, Matha Matayo (kulia), jinsi ya kutumia karatasi za kupigia kura. Wakwanza kushoto ni Ofisa uchaguzi, Michael Lazaro. 
Wananchi wa Mtaa wa Buguruni Kwamnyamani, Dar es Salaam, wakiwa wamesimama bila kujua hatima yao katika kupiga kura za kuwachagua Mwenyekiti na wajumbe wa Serikali ya mtaa huo leo, kutokana na karatasi za wagombea kutokamilika, huku Maofisa uchaguzi wakiwa wamekaa kwenye viti vyao bila kujua la kufanya.
Wananchi wa Kata ya Vingunguti, Dar es Salaam, wakiwa wamekusanyika kwenye Ofisi za Kata kwa ajili ya kwenda kupiga kura kuwachagua Wenyeviti pamoja na Wajumbe wa Serikali za Mitaa ya kata hiyo. Hata hivyo zoezi hilo halikuweza kufanyika kutokana na baadhi ya karatasi za wagombe kotokukamilika. Kulia ni Askari wa Polisi wakilinda amani kwenye eneo hilo. 
Wananchi wa Kata ya Ali Maua, Kijitonyama, wakipiga kura za kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa za kata hiyo, Dar es Salaam leo, huku mmoja wa wakala wa Vyama vya Siasa, akijaribu kumzuia mwananchi aliyedaiwa kuwa mkazi wa Mbagala (kulia aliyefichika), asipige kura kituoni hapo baada ya kukabidhiwa shahada za kupigia kura na Ofisa uchaguzi wa kituo hicho. 
















No comments:

Post a Comment