TANGAZO


Sunday, December 14, 2014

Hafla utoaji Tuzo za Taswa ulivyofana Diamond Jubilee

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Juma Pinto, akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo za mwanamichezo bora wa chama hicho, Dar es Salaam juzi.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar, Mwinyimvua Nzukwi, akimkabidhi tuzo ya mwanamichezo bora wa Taswa, upande wa Tennis wanawake, Rehema Athuman, wakati wa kutunuku tuzo hizo juzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said  Sadiki, akimkabidhi tuzo bondia Francis Cheka (kulia), baada ya kuibuka mwanamichezo bora katika mchezo huo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Juma Pinto, wakifurahia jambo, wakati mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Abeid Aman Karume, mama Fatuma, alipokuwa akiwaelezea jambo, wakati wa utoaji wa tuzo hizo juzi.
Rais wa Zanzibar, Dk. Shein akimkabidhi tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora wa Taswa, mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Abeid Aman Karume, mama Fatuma, kutokana na mume wake huyo kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya michezo nchini.
Wasanii wa bendi ya Kalunde, wakitumbuiza wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Mwanamichezo bora wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Dar es Salaam juzi.
 Wadau wa Taswa wakiwa katika hafla hiyo.
 Wadau wakiwa katika hafla hiyo.
Asha Kigundula (wa pili kulia), akiwa na mume wake, Majid pamoja na marafiki zake katika hafla hiyo.
Asha Kigundula (wa pili kulia), akiwa na mume wake, Majid pamoja na marafiki zake katika hafla hiyo.
 Wadau wa Taswa wakiwa katika hafla hiyo.
 Wadau wa Taswa wakipata chakula wakati wa hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Mshama, akipata chakula pamoja na wageni wengine. 
 Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mama Fatuma Karume, akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akizungumza wakati wa hafla hiyo, ambapo baadaye alimkaribisha Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuhutubia wanamichezo.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wanamichezo katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni, Alex Mshama, akiwa pamoja na wageni wengine 
 Vicky Kimaro akiwa pamoja na wadau wengine katika hafla hiyo.
Wadau wa Taswa, Athuman Khamis (kulia) na Mrocky Mrocky, wakiwa katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment